Ombi langu la pili (2) kwa Rais Magufuli

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
Baada ya siku chache kueleza ombi langu Kwa Rais Magufuli juu ya kuzitenga Sanaa na Michezo ziwe Wizara zinazojitegemea niliahidi kueleza ambavyo nadhani Serikali itajikusanyia Kodi nyingi kupitia Sanaa hasa baada ya kuonekana kukua Kwa Kasi zaidi Kwa 2019/20 (Rudi post zilizopita soma tena)

Tuanzie hapa

UANZISHWAJI WA VITUO VYA SANAA
Mimi nadhani kama Nchi tukaanzisha Vituo vya kufundisha Sanaa katika kila Wilaya nchi nzima, hii itasaidia kuibua Wasanii wengi wachanga ambao watakuwa wakipitia mikono ya Serikali, nachomaanisha katika Wilaya 150 nchi nzima tunahitaji Majengo 150 na kila kituo kitakuwa kikichukua Wanafunzi kwa Awamu (Mwaka 1), kuhusu gharama ya kusoma itakuwa ya kawaida ya kuwezesha Vituo kujiendesha, katika kila kituo wakiwa wanamaliza wanafunzi 40 kwa Mwaka. Tutakuwa na wahitimu wa Sanaa 6000, ambao Kati Yao kutakuwa na Bongo Movie, BongoFleva, Sanaa za Asili, NK.

Utaniuliza sasa Sangu hayo Majengo yatatoka wapi nitakujibu Wizara inaweza kuingia Makubaliano na Shirika la Nyumba la Taifa NHC, wakaikodisha Wizara baadhi ya Majengo ili kuanzisha vituo hivyo, na Wizara ikalipa kodi kama wanavyolipa wapangaji wengine.
.
Kuhusu Walimu wanaweza kupatikana kupitia Vyuo Vikongwe vinavyofundisha Sanaa (TASUBA, UDSM NK), hivyo kupitia hili Serikali inaweza kuungiza Pesa nyingi kupitia Vituo hivyi na Ikazalisha Wasanii wengi.
.
TAMASHA - TANZANIA ALL STAR FESTIVAL (TASF)
Tunaweza kuwa na Tamasha moja kubwa ambalo litafanyika kila msimu, na linajumuisha Wasanii wote, kama yalivyo Matamasha ya #JamaFestival #Fiesta #WasafiFestival na wananchi waingie kwa vingilio na Pesa zitakazo patikana zigawanywe, asilimia fulani ipelekwe kwenye vituo vya Sanaa ili kusaidia Wasanii wachanga, Asilimia nyingine liingie Wizarani na nyingine walipwe Wasanii.
.
SERIKALI KUWA WAKALA WA WASANII KWENYE MITANDAO YA SIMU
Kwa mujibu wa Ripoti ya TCRA ya Marchi 2020 Wanaomiliki Laini za simu nchini wako Milioni 48, tufanye wanaotumia huduma ya wimbo wa Msanii ni watu Milioni 20 Kwa siku ambao gharama ya wimbo Kwa siku 7 ni shilingi 150 Kwa hesabu unakuta Pesa zinazopatikana Kwa wiki karibia Milioni 300, ambazo Pesa hizi zikipita Serikalini ndiyo wapewe Wasanii.
.
Kwanini nimesema zipitie Serikalini itawekwa kanuni ambayo itaifanya Kampuni ya Simu iingie Mkataba na Serikali kwenye kuzitumia nyimbo za Wasanii, na Serikali pia itaingia Makubaliano na Wasanii ili kukwepa udanganyifu unaoweza kujitokeza.
.
Kwanini Makampuni yaingie Mkataba na Serikali nasi Wasanii direct kwa sababu Serikali inauwezo wa kupata Kwa urahisi Takwimu halisi za watumiaji wa Mitandao ya Simu na huduma walizotumia Ila Kwa Wasanii ni ngumu Kwa sababu wao wanapokea taarifa za Mitandao ya Simu ambao ndiyo wafanyabiashara wenzao kwenye hilo.
.
PESA KWENYE MEDIA ZINAVYOTUMIA NYIMBO ZA WASANII

Kwenye hili pia Serikali inaweza kutanya kwa kuangalia utaratibu mzuri ambao utakuwa umekubaliwa na pande zote.

Kwa leo niishie hapa toleo lijalo Nitaeleza fursa nyingine ambazo nadhani Serikali inaweza kuzitumia ili kupata Pesa nyingi zaidi kupitia Sanaa.
.
Nicheki Insta : FB : Twit : Sangu Joseph

#KijanaaMzalendo #IloveTZ
 
Mkuu andika barua ya wazi kwa Waziri husika.
 
Pamoja na hilo unaweza kushirikiana na vijana wenzako wenye maono mkaanzisha program tumishi kupitia maoni yako ikawa inawaingizia pesa upande huo huo wa muziki badala ya kutaka serikali ikusanye hayo mapato.
 
Ngoja kwanza tuone atakavyo amka ili kujua kama atayafanyia kazi hayo mawazo yako, au atayapotezea.
 
Back
Top Bottom