Ombi langu juu ya siku ya wafanyakazi (Mei mosi )

Cotton pamba

JF-Expert Member
Dec 16, 2020
303
208
Wakuu poleni na matanga ikiwa bado tunaendelea kuomboleza msiba mzito wa taifa, kwa kuondokewa na Rais wetu mpendwa Mh. John Pombe Magufuli ambaye Mungu kamwita.

Naomba sasa nigusie jambo kuhusiana na Mei Mosi ijayo. Ama hakika watumishi wa umma tumekuwa wavumilivu kwa kipindi kirefu bila ya mabadiliko yoyote ya maslahi, tuliendelea kuchapa kazi ili kuunga juhudi za kujiletea maendeleo katika taifa. Tena kwenye hili viongozi wakubwa wa nchi tunategemea mtoke na mtusifu sisi watumishi wa umma.

Kwako mama yetu kipenzi, Mh Rais Samia ,mapema hii tunaomba mwaka huu basi neema iwepo kwa kundi hili. Its been a while mama yetu toka tumefurahishwa na Serikali yetu pendwa.

Maisha yetu sio mazuri sana yana ma-gape sana. Mikopo inatutesa hasa hii ya elimu ya juu ndio balaa, mzee wetu alisema bado yupo ko tusubir sasa hayupo uliyepo ni wewe, hope mwaka huu mzee alipanga jambo juu yetu watumishi basi Mama yetu pindi uingiapo offisini kale ka file ketu anzanako.

Sote tunajua jinsi mungu alivo wajalia huruma mama zetu, watumishi wa umma wataifa hili tunakupenda mama etu, tunamwomba mungu akupe hekima, busara, upendo kwa watumishi wa umma na wananchi wote wa tz kwa ujumla.

Umetuona wa Tanzania kwenye msiba wa mpendwa wetu tulivo wamoja na nikuhakikishie sisi tunaipenda nchi yetu pamoja na viongozi wake.

Tatizo ni hii hali ya kusahaulika tena kwenye jambo la msingi (maslahi) inavunja moyo kiukweli.

Nimalize tuu kwakusema tunakupenda mama yetu na daima tutachapa kazi ila tukumbuke mama.
 
Kwa nn mkuu
sijawahi kuona mtumishi wa umma akijaribu kusema atafanya nini kwenye eneo lake la kazi,ila nachoona wengi wanadai maslahi lakini si kusema lolote kuhusu utendaji kazi wao;
yaani nawaza namkuta mtumishi wa posta,TTCL,tanesco au dawasa yuko anadai maslahi muda huo naona huduma mbovu na ya hovyo kabisa ndio anatoa;
mimi mi mtumishi wa umma pia,ila tujaribu kuboresha utendaji kazi wetu,raia wengine pia ni watu;
sikupingi ila tutimize sehemu zetu pia;
 
Stupidity of the highest order! Mtu afanye kazi asidai ujira wake? Kama waona poa nenda kajitolee wewe kulingana na fani yako ewe mzalendo !!
kama umeandika hivi ukiwa na akili timamu,basi jitafakari,hata hayo madai yako yatakua kama ufikirivyo;
JF imekua ni sehemu ya watu kutukana na kuleta uhasama kisa hujui unamjibu nani,kama mtumishi wa serikali kabisa ndio umeandika hivi,ninaweza kusema tuna safari ndefu sana kufikia fikira njema na salama;
jibu mtu kwa hoja,nashukuru mleta mada ameniuliza kwanini,na nimemjibu vema;
nisiseme mengi,kama hujaelewa mchango wa mtu,heri kukaa kimya,waweza kuandika kuonekana una hekima na elimu,kumbe ndio unazidi kufungua upeo wa watu juu yako;
asante kwa mchango wako;
 
Mimi naomba siku ya mei mosi atukumbuke tusiokuwa na ajira!

Tumepigika mno huku mtaani jamani!
Angalau na sisi tufaidi kidogo keki ya taifa kama nyinyi!
 
Back
Top Bottom