_ BABA _
JF-Expert Member
- Nov 23, 2009
- 203
- 20
Habari wandugu.Kati ya miezi ya sita mwishoni na saba katikati mwaka jana Tanapa walitangaza nafasi za kazi kwenye idara tofauti tofauti, rafiki zangu wawili wanaishi mkoa mpya wa Katavi walituma maombi kuomba moja wapo ya hizo kazi kulingana na sifa zao,wamenambia toka kipindi watume maombi wamekua wakifuatilia kwenye magazeti pamoja na tovuti ya Tanapa kuona kama wameitwa kwa ajiri ya interview ila hawajawahi ona majina ya watu walioitwa kwa ajili ya interview, hivyo wakaniomba nijaribu waulizia kama Tanapa walisha ita watu kwa ajili ya interview sababu mimi waga natembelea sana Arusha, ila mimi sina connection kabisa na watu/mtu wa Tanapa ambaye ningeweza muuliza, hivyo ninachoomba ni:-
Kama kuna mtu anahabari yeyote kuhusiana na hizo nafasi zilizotangazwa mwezi wa 6 na 7 mwaka jana nitashukuru sana akinijulisha kama walishatoa hiyo short list kwa ajili ya interview au kama kuna watu/mtu wa huko Tanapa ningependa sana wakinijuza ili niwape majibu hao rafiki zangu.
Natanguliza shukrani.