mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,037
TCU ilipandisha cut off points kwa ajili ya kujiunga na kozi za afya kwa digrii na kuwa 8 yaani C, C na D badala ya D, D na S. Kwa maoni yangu sioni ulazima wa kutaka MTU apate D ya physics kama kigezo cha kusoma kozi ya afya. Masomo ya msingi kwa kozi za afya ni chemistry na biology. Kwa hiyo wangerudisha kigezo cha awali kuhusu physics cha kuhitajika kupata angalau S ya physics. Kwa hiyo kigezo kiwe C, C na S point 6.5. Madaktari bingwa tulionao Leo wengi walipata S ya physics na hilo halikuwa kikwazo kwao kusomea udaktari au pharmacy. Hiki kigezo cha sasa kinaharibu sana ndoto za watu na baadhi ya vyuo vinaweza kuwa vinakosa wanafunzi!!! Chonde chonde tazameni upya vigezo hivi. Watoto ndo mwezi ujao wanaanza mitihani yao! Ni vizuri kuweka vigezo kabla hawajafanya mitihani ya kidato cha sita.