Ombi kwa Mheshimiwa Rais baada ya Uchaguzi

astranaut

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
1,276
1,021
Mimi kama Mtanzania mzalendo na mpenda maendeleo, katika kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa Taifa. Ningependa kutoa rai kwa Mh Rais pindi atakapochaguliwa kwa mara ya pili kuelekeza nguvu zaidi katika miradi mikubwa anayo itekeleza hasa hasa mradi wa umeme na reli ya kisasa. Kwani endapo miradi hiyo itashindwa kukamiika mapema katika kipindi cha ungozi wake basi sio rahisi tena kwa atakae mrithi kuikamilisha kwa wakati kutokana na kwamba inagharim fedha nyingi huku ikihitaji juhudi za dhati katika kukusanya mapato.

Hiyo mingine midogo midogo atakuja mwingine kumalizia wewe deal na hiyo kwanza ya kimkakati itakayo acha regecy kwa vizazi na vizazi kukukumbuka, kwa sababu kama mradi wa umeme unahitaji kiongozi mwenye uthubutu wa juu kutokana na presha ya wakubwa kuupiga vita huo mradi. Mradi huo umepingwa nje na ndani ya nchi eti unaharibu mazxingira hivyo basi itakua ngumu kama hautakamilika katika kipindi hiki cha miaka mitano kukamilika baada ya yeye kumaliza muda wake.

Pia mradi wa reli ya kisasa kwa makadirio ya kihandisi inakadiliwa kuchukua miaka 15 kukamilika na ni mradi unaochukua hela nyingi sana huku nyuma kukiwa na vijembe na mapingamizi ya wafanyabiashara wenye malori yao ya kusafirisha mizigo. Hivyo kuna hati hati ya atakae fuatia kama mradi kweli utachukua miaka 15 kutokamilika kwa muda lio panwa na ikachukua hata miaka mingine 40

Hivyo basi mh kama utachaguliwa kwa mara nyingine tena mimi inanipendeza kujuikita zaidi na hii miradi kwanza, pesa ambayo umetengea kunua meli maziwa makuu japo ni muhimu lakini sio muhimu zaidi kama ilivokua hii miradi ungeilekeza kukamilishia hii miradi ili hao wengine watakao fuata watafanya hayo madogo madogo kulingana na uwezo wao.
 
Kweli Ujinga wetu Unakithiri jamani.

Hivi unaemwimbia mapambio akifa leo itakuwaje?

CCM imeshindwa Kutengeneza Taasisi na Mifumo imara ya Kitaasisi. Bila kuwa na Taasisi Imara ni hakuna kitu.

Nyerere aliacha viwanda Ndege mashamba nk. Lakini vyote vilikufa kwa kushindwa kutengeneza Taasisi imara.

Bila Taasisi Imara Jiwe anapoteza Muda tu.
 
kwani reli na baadhi ya shule kongwe unazo tumia leo vilijengwa na nani?

Nina mashaka na hiyo miradi kukamilika kwa 100% ndani ya miaka mitano. Fahamu hiyo miradi miwili mikubwa hakuna hata mmoja uliofikia robo ya inavyotakiwa. Hivyo kwenye figure ya miradi yote miwili ambayo ni 15t+ hajatoa hata 7t+, je ni wapi atapata 7-10t kwa ajili ya kukamilisha hiyo miradi ndani ya 5yrs, huku mambo mengine yakiendelea?

Hayo mengine anayoahidi kwa sasa labda miradi ya chini ya 200b, lakini sio zaidi ya hapo. Sehemu ambazo anaweza kukopa ndio kashazimaliza, na makusanyo ya ndani sioni yakifanikisha hilo. Sidhani kama alishauri namna nzuri ya kufanya hiyo miradi, na kama aliamua mwenyewe kwa jeuri, basi yajayo yanafurahisha.
 
Kweli Ujinga wetu Unakithiri jamani.

Hivi unaemwimbia mapambio akifa leo itakuwaje?

CCM imeshindwa Kutengeneza Taasisi na Mifumo imara ya Kitaasisi. Bila kuwa na Taasisi Imara ni hakuna kitu.

Nyerere aliacha viwanda Ndege mashamba nk. Lakini vyote vilikufa kwa kushindwa kutengeneza Taasisi imara.

Bila Taasisi Imara Jiwe anapoteza Muda tu.
kipi kianze kati ya taasisi imara na miradi ya maendeleo? kipi kina umuhimu zaidi
 
Back
Top Bottom