Ombi kwa mhe. Rais magufuli kwa wamachinga

basiri

Senior Member
Aug 31, 2018
168
149
Kwanza nianze kwa kumpongeza mhe.rais kwa utaratibu wa kuweka vitambulisho kwa wajasiliamali walio na mtaji chini ya mil4 kwa mwaka ili nao wachangie mapato ya nchi

Mheshimiwa rais utaratibu uliopo ni mzuri lakini changamoto zake ni kubwa mhe.utagombana na watendaji wako bure kwa sababu hawa wajasiliamali waliopo katika masoko yetu tunawategemea sana ili kuendesha masoko yetu utaratibu tuliojiwekea uko hivi ;
●Kuna kiasi kidogo cha kuchangia usafi wa soko
●Kuna kiasi kidogo cha kuchangia ulinzi wa soko
Hayo hapo machache hapo juu ni mhimu sana na ukizingatia hiyo kodi kidogo ya soko haipatikani kupitia vitambulisho vya ujasiliamali


Ombi langu kuwekwe utaratibu ili hawa wajasiliamali wasisumbuane Na uongozi wa soko katika hiyo elfu 20/= ya kitambulisho kukatwe asilimia kidogo ili kuchangia kodi hizo kidogo za soko ambazo ni pamoja na usafi wa soko ,ulinzi wa soko

Elimu itolewe kwa wajasiliamali juu ya kuendeshaji wa masoko yetu yanategemea sana hizo kodi kidogo au wao wenyewe wajasiliamali wajipange kufanya usafi au ulinzi

Changamoto wajasiliamali hawana ushirikiano ili kutekeleza hayo kwa umoja wao

Mwisho
Elimu zaidi itolewe kwa wajasiliamali ili kuondoa migogoro na watumishi wako
 
Back
Top Bottom