Ombi kwa Bernard Membe

Acha kumtisha wewe kwani we pia si ulimuita fisadi alipokuwa CCM???
Usichezee ugonjwa hata siku moja ndugu yangu...tema mate chini yasikukute, mimi siyo chadema and will never ever be! Lakini siwezi kunyanyua mdomo wangu kumkufuru Mwenye Enzi Mungu kumcheka mgonjwa...ehh Mola niongoze milele
 
hata kama alikula hizo hela, lakini ukweli uko palepale, kamzidi jamaa mbali sana kwa kila kitu, angelikuwa rais tungepiga hatua haraka sana.
Kuna baadhi ya mambo yananifanya najiuliza maswali kadhaa kwa sababu ya hoja yako hii.
1. Haumkubali rais aliyepo madarakani kwa kipindi kingine?
2. Kama ni hivyo, membe na huyo rais wa sasa wote ni wana ccm kwa sababu gani wasishindane ndani ya chama chao kisha huyo membe akachuana na wagombea wa upinzani?.
3. Haukubaliani na sera /ilani ya uchaguzi ya ccm ambayo inatekelezwa na rais aliyepo madarakani kwa sasa?

Hebu nisaidie ufafanuzi kwa mambo hayo kisha niendelee na maswali mengine mkuu
 
Huyo hiyo Eddo hata akae 30 no problem lazima akawang'oe Team Bashite Zero na PhD hewa
 
Mwandishi big up xna, constructive ideas itabd nkutafute pm.
 
Sijawahi kuona hoja ya kijinga kama hii
Wanafiki utawaona kwa maneno na matendo yao tu; leo unajifanya maisha ya JK yalikuwa mazuri wakati ulishiriki kumchafua!? Kweli hamjitambui na ndo mana mnasahau mliongea upumbavu kiasi gani enzi za utawala wa Mzee wetu JK. Eti ung'eng'e dili mbona we unaeujua umeshindwa kuongoza hata Kata yako tu sembuse Nchi?
 
Bora tumpe mzalendo wa nchi hii
Bernad Camilius Membe
Yanayotokea sasa ni hofu ya kuogopa kivuli chake
Huo ndiyo mtindio wenyewe wa ubongo, kwani wakati mnamuita team JK na kwamba wanachaguana na kupeana madaraka hamkumuona anafaa ila leo ndiyo akili zimewarudia siyo????
Kweli chizi karogwa tena.
 
Mleta mada umeleta hoja nzuri ila sidhani kama wakati huu ni sahihi. Utasababisha Mzee Membe aanze kusumbuliwa tu. Hii hoja ingekuwa vizuri zaidi ungeileta mwaka2019 mwishon au 2020 mwanzoni

Mwaka 2019 ni mwaka wa kupiga kura ya maoni ili JPM aendelee hadi 2035

Mnaodhani upinzani una nafasi 2020 mnajisumbua bure tu.

Upinzani Tanzania umebakia kuwatetea wauza unga, wakwepa kodi, wahujumu uchumi na saa watoroshaji mchanga wenye madini.

Membe kwa sasa ana 64 si mbaya, ila alikosea hesabu kumwachia Nape jimbo la Mtama katika mipango yao.

Ila bado ana sauti ya kuweza kusikika ndani ya NEC.
 
Ogopa sana kuwapa nchi watu waliowahi kuwa mawaziri wa mambo ya nje au mabalozi hawa huwa ni vibaraka wa mataifa makubwa na wengi wao huingiza nchi katika mikataba mibovu chukulia mfano Tanzania leo hii mikataba mibovu iliyo yote ilifungwa wakati nchi ikitawaliwa na waliokuwa mawaziri wa mambo ya nje.

Mimi sipendi Sera za magufuli lakini kwa hili ni bora magufuli Mara 100 kuliko Membe
 
membe ana mapungufu mengi sana, lakini ndiye rais bora kuliko wanaccm wooote, kwanza anajua kiingereza, elimu yake sio magumashi, ana utaalamu na diplomasia, ni afisa usalama wa taifa, halafu ana akili.
Wewe sio kada tuulize makada
 
Watanzania
Wapinzani
Wakiingia
Ikulu
Dunia
Itawacheka


Huwezi ukawakabidhi wapiga dili nchi
Mawe yataongea
 
Huyo jamaa kichwa chake kimeingiwa virus inabidi kuki-format kabisa
 
membe ana mapungufu mengi sana, lakini ndiye rais bora kuliko wanaccm wooote, kwanza anajua kiingereza, elimu yake sio magumashi, ana utaalamu na diplomasia, ni afisa usalama wa taifa, halafu ana akili.
Unajua kuwa Membe alipata Div 4 form four?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…