Ombaomba, Kina Mama

malikafif84

Member
Feb 6, 2013
39
31
Idadi ya kina Mama wanaoomba katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan inaongezeka kila mwaka, kuna kitu cha kujifunza na kufuatilia kuhusu maisha yao! Kuwasaidia peke yake haitoshi.
 
Kilimanjaro hatunaga huo utaratibu, wazee wote wanatunzwa na familia zao tena kwa mapenzi ya hali ya juu hakuna kuzurura kuombaomba. Pia akina mama wa Kilimanjaro hasa pale Moshi mjini ndio "chinga".
Poleni mikoa ambayo akina mama wanasubiria mwezi wa Ramadhan na kuanza kupita kwenye mabaa, maduka ya wahindi na sehemu zingine kuomba
Mh acha uongo wa wazi wale tunaowakuta pale mjin CRDB wamehamia toka mkoa gan
 
Kilimanjaro hatunaga huo utaratibu, wazee wote wanatunzwa na familia zao tena kwa mapenzi ya hali ya juu hakuna kuzurura kuombaomba. Pia akina mama wa Kilimanjaro hasa pale Moshi mjini ndio "chinga".
Poleni mikoa ambayo akina mama wanasubiria mwezi wa Ramadhan na kuanza kupita kwenye mabaa, maduka ya wahindi na sehemu zingine kuomba
Kilimanjaro ipi unayozungumzia? Kutoka stendi hadi Mawenzi kuna idadi kubwa ya ombaomba, pia Njia ya kwenda UCHUMI house kuna ombaomba wa kutosha.
 
Hivi kuna mtu anayependa kuwa ombaomba? Sidhani. Ukipenda msaidie, hupendi acha! Tunakunywa mipombe na kuwa na matumizi ya hovyohovyo kila siku. Sasa anatokea mtu anakupiga mzinga wa shilingi mia tano tu unahamaki? Aaaaa mkuu, hebu tafakari mpendwa!
 
Mnawaendekeza.! Kama mtu ana afya na viungo vilivyokamilika hapaswi kusaidiwa.
 
IMG_6371.JPG
Mtu aliyesimama kivilini hawezi kujua ukali wa jua....bali aliyesimama juani ndiye ajuaye....

Kukamilika kwa viungo kwa mwanadamu hakuewezi kukamtoa kwenye ufukara bali ni yule aliyejaaliwa na utashi katika matumizi ya viungo hivyo..........

Akili kila mtu anazo isipokuwa ni wachache wenye uwezo wa kuzitumia akili zao bara bara......

Ni sawa na mtu anayekufa na njaa hali ya kuwa ameshika chakula mkononi.......


Kuomba omba kunaijenga akili yako kwenye utegemezi.....
 
Wachache wenye shida... mfano mwanza pale wamejaa ukiwapa kiasi flan hebu nenda mwisho ya mto mirongo ziwan ukaone wanavyopiga pombe za kienyeji uko... wengne ishakua ni biashara yao.. unamkuta maza na watoto town kati mpk wana sufuria wanapika alafu omba omba.. benki kuu pale kwa mbele kama crdb mwanza ni kero wamama wamekaa vitoto vidogovidogo vinakimbilia watu tena vinaomba kwa lazima mama zao wanapiga story tu vikipata chapu vinapeleka kwa mama zao.
 
Back
Top Bottom