Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,094
- 866
Tunaishi kwenye dunia ambayo ni rahisi sana kuwa na uelewa ‘mparazo’ wa mambo lakini huna mizizi inayoushikilia uelewa huo. Unaenda YouTube, kwa mfano, unaangalia maelezo mafupi ya mtu akifafanua jambo na tayari unaamini unajua kila kitu kuhusu jambo hilo. Siku hizi unaweza hata kuangalia vipande vifupi fupi vya maelezo ya dakika moja moja Instagram na tayari unaamini umeshazama.
Tatizo la dunia hii ya ‘elimu mcharazo’ ni kwamba unaweza kufika mahali ukaanza kuamini huhitaji kabisa kuzamia kitu ukielewe kwa mapana yake. Unaanza kuamini dakika mbili za ‘muhutasari’ wa maarifa kule Instagram ndio ukweli mkamilifu. Unaanza kuamini ‘prompts’ za aina ya madawa kwenye Akili Ige (AI) zinakufanya uwe sawa na mwenzio aliyesomea madawa. Tumeanza kuishi kwenye dunia ambayo unachofikiri unakijua, kwa uhakika kabisa, ni kivuli tu cha maarifa.
Sikatishi tamaa teknolojia na maendeleo yanayorahisisha ujifunzaji. Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba pamoja na umuhimu wa enzi hizi za ‘uholela’ wa maarifa, ambapo kila mtu anapata ujasiri wa kuwa bingwa ‘mcharazo’ wa chochote anachotaka, bado ni muhimu kuwa na uwezo wa kujifunza na kufuatilia jambo katika kina chake ukalielewa. Kuwa na ‘taarifa’ nyingi zinazorahisha jambo gumu ni vizuri lakini hakuwezi kulinganishwa na uelewa wa kina wa misingi, nadharia, falsafa nyuma ya jambo moja unaloweza kusema unalielewa vizuri.