fredy mziray
New Member
- Sep 20, 2012
- 4
- 0
Ndugu watanzania wenzangu, nasikitika kuwaona ombaomba wengi katika eneo la Ubungo mkoani Dar es salaam na maeneo mengine ya mikoani wakiwa katika maeneo hayo kila siku. pamoja na kuwasaidia fedha kidogo msaada huo hautoshi kuwaondoa pale walipo kutokana na hali zao za kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi za kutumia nguvu.
Wakati serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI ikipitisha bajeti zenye kutumia fedha nyingi kwa kulipana posho na mishahara minono kwa watumishi wa ngazi za juu hasa wabunge na mawaziri inatakiwa pia kuwakumbuka walemavu wale wasio na msaada wowote wa kuwafanya waishi kama watanzania wegine kwa kuwaanzishia vituo maalumu ambapo watapata huduma na kutunzwa kwa gharama za serikali.
Naomba ndugu wananchi na wabunge kuweza kuishinikiza serikali ili iweze kulifanyia kazi swala hili kwani hawakupenda kukaa chini na kunyeshewa na mvua wakiomba msaada.