Omar Al Bashir tena

Omar Al Bashir tena

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,377
Reaction score
38,266
Huku K WEST, Huku OMAR AL BASHIR!

K. WEST ameshinda tuzo inayokwenda kwa jina: TUZO YA KAZI ZENYE MAFANIKIO, nchini MAREKANI, katika tuzo hiyo, WEST amepewa nafasi ya kusalimia watu waliojaa ukumbini humo na katika salamu zake, ameahidi KUGOMBEA URAIS WA USA 2020!

Kuonyesha kuwa yupo makini na akisemacho, West amewaambia mashabiki lukuki kuwa, wengi watadhani AMEVUTA BANGI kabla ya kuingia ukumbini, lkn si kweli!

Kwa upande wa mwengine, Rais wa Sudan, Omar Al Bashir, kesho anaondoka Sudan kuelekea CHINA kwa ziara ya siku kadhaa, kuadhimisha miaka 75 ya kumbukumbu za vita VYA dunia nchini humo.

Omar Al Bashir anasafiri kwenda CHINA huku akiwa anasakwa na ICC na kumbukumbu zinataja kuwa safari yake ya South Africa ilikuwa mojawapo ya safari zake za mafanikio kipindi hiki akiwa na warranty ya kukamatwa.

Haitegemewi CHINA kufanya kitu chochote kibaya kwa Rais huyo kutoka Africa, hasimu wa MAHAKAMA ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC
 
Back
Top Bottom