Olympus Has Fallen VS White House Down

Loy MX

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2012
Posts
1,253
Reaction score
313
Kwa wadau wa movie
Filamu mpya ya Anton Fuqua THE OLYMPUS HAS FALLEN inaangukia kwa star Gerald Butler anayecheza kama mwana usalama aliyepoteza ajira yake kutokana na kifo cha first lady kilichosababishwa na ajal ya gari.. Lakini anapata nafasi nyingine ya kurudisha heshima yake pale anapojaribu kuiokoa ikulu ya Marekani kutoka kwenye mikono ya magaidi.

Miezi michache baadae Director Roland Emmerich nae anatoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la WHITE HOUSE DOWN yenye mwonekano na mahadhi kama filamu ya the olympus has fallen katika movie hii anajaribu kuchanganya ladha ikiwamo kumweka Rais mwenye ngozi nyeusi (Jamie Foxx) pia anamjumuisha Channing Tatum ambae anacheza kama mwana usalama anae jaribu kuiokoa ikulu ya marekani kutoka kwenye genge la magaidi..

Movie zote mbili ni nzuri lakini mi nimeipenda zaidi White house down kwa jinsi walivyoweza kulchezea limousine (The Beast) ya Mr Prezidaa.. Ipi ni movie nzuri kwako?
 
Olympus has fallen is my favourite,super actions na hata utekaji wao wa white house uko more complicated
 
Olympus has fallen is my favourite,super actions na hata utekaji wao wa white house uko more complicated

Sure Mkuu sababu kwenye WHD haikueleweka silaha ziliingiaje ikulu..
 
Siku hizi nimekuwa mvivu sana kuangalia haya makitu
White house down ninayo nitaiangalia leo aisee naona inasifiwa sana
 
whitehouse down uongo mwiingi

eti rais ana kimbizwa na magaidi mbele ya white house huku jeshi linatazama kusubiri order...
 

Sijaiona bado White House Down!! Ila Olympus Has Fallen!! Dahhhhhh ni Balaaaaaa!!!!!!!!!
 
Ngoja nicheki pia.
Ila wakuu kuna series ya scandal nayo nimeikubali sana kuanzi season 1 episode 8 duh.
Kuna ishu moja kama ya snowden kabisa.
ova walijua kwanza ndio wakatoa. Ikanifanya nifikirie sana msemo wa lisemwalo lipo kama halipo basi laja!
Human cloning lazma ishafanyika nahis.
 

Mkuu hiyo scandal naipata wapi?nikitaka kununua.
 
Daah! Mkuu kudownload inasumbua sana na hizi bundle zetu za kuungaunga. Mkuu nikupm nije kunyonya kwako kama upo dar?

kaka kama una line ya voda unajiunga na wajanja night sh 200 tu kuanzia saa 4 usiku kisha unapakua hayo makitu kiulani kabisa maana unaiacha inadownload unaenda zako kulala ukiamka asbh unakut mzigo tayari.Nimeshapakua nyingi sana tena zenye quality ya HD kwa dizaini hiyo
 

Daah! Sina kaka. Natumia sasatel inakula hela balaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…