Olle milly kuvuliwa uanachama ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Olle milly kuvuliwa uanachama ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibakwe, Jun 8, 2011.

 1. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MGOGORO ndani ya CCM Mkoa wa Arusha umeshika kasi mpya baada ya Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa za chama hicho mkoa kudaiwa kumvua
  uanachama Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) Mkoa, Bw. James Ole Millya.

  Pia vijana wengine watano wa umoja huo wanaodaiwa kuwa vinara wa mgogoro nao watakumbwa na rungu hilo baada ya kamati hizo kutoa mapendekezo ya kufukuzwa uanachama kwa kitendo chao cha kushadadia kuondoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Bi. Mary Chatanda.

  Habari kutoka ndani ya vikao hivyo ambazo zimethibithswa na baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa sharti la kutotajwa majina, zimedai Kamati hiyo iliyoketi mwishoni mwa
  wiki ilitoa mapendekezo yake kuwa Mwenyekiti huyo anayedaiwa kuwa kinara wa mgogoro huo pamoja na vijana hao avuliwe madaraka.

  Vyanzo hivyo vilidai kuwa kikao cha kamati hiyo pia kilihudhuriwa pia na wajumbe kutoka Kamati ya Maadili ya Taifa ikiongozwa na Kanali Mhando na wajumbe wawili kutoka UVCCM Taifa ambao ni Bw. Seif Malinda na Mzee Mipoko kilichokaa kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

  Mapendekezo hayo baada ya kuridhiwa na wajumbe hao yalifikishwa katika Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa, kilichofanyika siku moja baadaye na kuridhia mapendekezo hayo, hivyo kusubiri kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kinachotarajiwa kukutana Jumamosi wiki hii kwa ajili ya maamuzi zaidi.

  Vyanzo hivyo vimewataja majina ya vijana watano kati ya 11 waliohojiwa siku hiyo, kufuatina mgogoro unaotokana na falsafa mpya ya CCM ya kujivua gamba ambapo makada waandamizi wa chama hicho, aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge wanashinikizwa kuachia ngazi zao.

  Baadhi ya sababu zilizoelezwa za kuwajibika kwa Bw. Milly
  Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Bi. Mary Chatanda.

  Wadadisi wa mambo ya siasa mkoani hapa wameeleza ya kuwa iwapo hatua hiyo ya kuwavua uwanachama vijana hao itatekelezwa itazidi kuchochea na kupanua mgogoro huo ambao ungeweza kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia na kupunguza ufa ndani ya chama hicho.

  Lakini kundi lingine linatoa matamshi mazito dhidi ya makada hao na kueleza kuwa wanapaswa kuwajibika kwa tuhuma zinazowakabili na kwenda mbali zaidi na kumtaja Bi. Chatanda ni lulu ya chama mkoani hapa na hapaswi kuondoka.

  SOURCE;MAJIRA
   
 2. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Huyu si ndo aliwahi kugombana na Ole Sendeka mpaka kesi ikaenda mahakamani?
   
 3. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama wasemavyo walinzi wa kimakonde; CCM wakikaa nchale, wakisimama nchale. Wasivue uanachama baadhi na hasa wale wadogo wawavue wakubwa kuanzia kule juu.
   
 4. Mwache77

  Mwache77 Senior Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Ndio yeye uyo kijana ka2mwa hata ule ugomvi alitumwa 2 ngoja tuone hy jmamoc
   
 5. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wa Arusha tukiona hayo ndiyo furaha yeti maana kupitia Chatanda watu walikufa.
   
 6. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ndio tatizo la kuwa kibaraka katika siasa, ata akivuliwa uanachama hana impact yoyote kwenye chama chake na kwa kusimama kwake kwenye udhalimu amekosa cha kujivunia na kumfanya awe lulu kwa wananchi, shame..
   
 7. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Sio yeye, bali aliyegombana na Ole Sendeka ni Lowassa kupitia mgongo wa huyohuyo James Millya....! Kibaraka huyo mkuu...!

  Mkuu Avatar yako vipi? Mbona kuna mawili?
   
 8. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilifikiri wataanza kwa kuvua magamba yale makukuu na makubwa kwanza kumbe wameanza na vijigamba vidogovidogo tena vipya tuu? Kaaazi kweli kweli
   
 9. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Watadai mgogoro huo umechochewa na chadema,
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Za mwizi 90, wakati wake umefika:shut-mouth:
   
 11. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  The comedi is good
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wanaoga kwenye matope.
   
 13. MANI

  MANI Platinum Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,411
  Likes Received: 1,870
  Trophy Points: 280
  Watasafishika kweli mkuu ?
   
Loading...