Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,608
Aliyekuwa Mbunge wa Simanjiro na mwanasiasa mkongwe, Christopher Olesendeka, amesema wagombea wa Urais wa Tanzania kutoka vyama vya upinzani hawawezi kulinganishwa na mgombea wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Akizungumza katika kampeni za ubunge jimbo la Mbulu Mjini mkoani Manyara hivi karibuni, Olesendeka amesema wananchi wasifanye makosa ya “kuchezea shilingi chooni” kwa kuchagua wagombea wasiokuwa na uwezo.
“Hii nchi iko salama kwa Samia, lakini ngoja niwaulize — Samia anashindanishwa na nani? CHAUMMA? Mnamjua huyo mgombea wa chama hicho? Amewahi hata kuwa diwani? Au ACT, au kitu kingine kinaitwa NRA, inajulikana kweli? Mimi nimekuwa Mbunge muwaambie hizo kata msichezee shilingi kwenye tundu la choo lakini nataka niwaambie upinzani hauwezi kushinda kama hakuna WanaCCM walionuna”, amesema Olesendeka. A
meongeza kuwa wagombea wote wanapaswa kuomba kura kwa unyenyekevu bila majivuno, na kwamba vijana wanaozungumzia siasa bila kuelewa historia, mila na misingi ya CCM hawana hoja za msingi. Olesendeka pia amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura, na kuchagua “kile kilicho bora” kwa mustakabali wa taifa.