"Ole wako uzitumie vibaya" haikuwa kauli sahihi kutoka kwa rais kumueleza Meck Sadick hadharani!

Jana kwenye hotuba ya John Magufuli (rais wa Tanzania) alitumia kauli isiyo na weledi kutoka kwenye cheo alicho nacho kumueleza mtendaji wake ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadick! "Nitakupatia hizo fedha na OLE WAKO UZITUMIE VIBAYA" kauli ya "Ole wako uzitumie vibaya" ingawa hamtasema wala kuongea ila kiukweli ilimfedhehesha sana Meck Sadick!

Kwanza Meck Sadick kiumri ni mtu mzima sana kwa Magufuli! Lakini pia ni aina ya watu ambao wamestaharabika! Ile kauli rais aliitoa kama anamueleza kijana mdogo na au mwanaye!

Pili haipendezi kuanza kujenga malengo hasi na inaonyesha kuwa kuna mashaka fulani!

Rai yangu kwa rais; emb ajifikirie kuwa yeye angekuwa ndiye Meck Sadick kwa kauli ile angeipokeaje? Ndiyo maana vyuo vinafundisha communication skills! Ile CL111 pale thietre za UDSM hiyo ndiyo kazi yake! Uongee lipi ukiwa wapi na kwa nani!

Hizi kauli za kutishana kabla hata kazi haijaanza kwa kweli hazijengi! Zinazaa uoga na kutokujiamini! Magufuli atazame mfano wa mawaziri wake walivyokwama! Hii ni kutokana na uoga aliowajengea!

Baada ya kuambiwa hivyo what did the RC do? si uliona alicheka sana, meaning that the message did not carry any weight
 
Hii inaonyesha kwa kiasi gani wapinzani wa JPM wamekosa cha kusema kiasi kwamba wanaangalia hadi his choice of words. Ili mradi ujumbe umetumwa, umefika na kueleweka, the rest do not matter. Kinachotakiwa ni matokeo chanya. Hata ukitumia lugha laini lakini matokeo hayaonekani utakuwa kiongozi wa ovyo tu. Go go JPM, tuko nyuma yako.
 
Mbona yuko sawa tu bana tena hyo meck bas tu huwez kuwa mkuu wa mkoa tena dar yenye mapato makubwa kias kile na una mkoa mchafu nadhani kuliko yote hapa nchin maana yake nn? Hakuna kitu hapo nae ni jipu tu,kauli nzur sana hiyo,rais anajua kila kitu mpaka kutoa kauli hiyo
 
Kuheshimiana na ustaarabu wa kiongoz mkuu kwa viongozi wa chini yake ni kitu muhimu, magu hawezi kuongoza peke yake

Mkuu nakubali kiongozi yeyote wa ngazi ya juu kama raisi hawezi kuongoza peke yake.Meck Sadiki amekuwepo kwenye uongozi kwa muda mrefu kiasi cha kuwaelewa viongozi wengi akiwemo na Magufuli. Vivyo hivyo nae raisi ameongoza kama mbunge na waziri kwa kipindi kisichopungua miaka ishirini nae anauelewa utendaji wa viongozi wa nchi na hali ya sasa ya nchi na kinachotakiwa kufanyika.Tukubaliane siku za nyuma tulikuwa tunaomba kumpata kiongozi mkali,mtendaji na mwenye maamuzi ya haraka kwa wakati. Nakubali pia kuwa kwa umri wa mzee Meck Sadiki hatakiwi kuelekezwa/kuagizwa kwa lugha kali bali lugha ya staha. Kwa tunaomfahamu raisi Magufuli hili kwake ni maumbile na sio makusudi na ndivyo alivyoumbwa. Chukulia mfano wa mzee wetu Mkinga kwa wanaomfahamu ni mtu mwenye uwezo mkubwa na anaelewa mengi ya nchi hii na jinsi ya kuyatatua. Tatizo kwake ni katika kuchangia utadhani anagombana. Ila sikiliza kinachomtoka kichwani utamkubali. Haswa haya masuala ya bandari ana ufahamu wa hali ya juu mianya iliyopo inayochangia wizi na jinsi ya kuenenda.Kuna michango nilisema waziri mkuu wetu angeweza kumwita ofisini na kumsikiliza ila amvumilie ile sauti kwani nae kwake ni maumbile tu na sio makusudi.
 
Kwa mahali nchi ilipofika hakuna kucheka na kima,mtu mzima ndio mdudu gani?we unadhani muhimbili angecheka cheka saivi mama na dada zetu si wangeendelea kulala chini huku maji ya chooni yakitiririka.VIVA PAUL MAKONDA mnjonge myongeni lakini haki yake mpeni.
Jana kwenye hotuba ya John Magufuli (rais wa Tanzania) alitumia kauli isiyo na weledi kutoka kwenye cheo alicho nacho kumueleza mtendaji wake ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadick! "Nitakupatia hizo fedha na OLE WAKO UZITUMIE VIBAYA" kauli ya "Ole wako uzitumie vibaya" ingawa hamtasema wala kuongea ila kiukweli ilimfedhehesha sana Meck Sadick!

Kwanza Meck Sadick kiumri ni mtu mzima sana kwa Magufuli! Lakini pia ni aina ya watu ambao wamestaharabika! Ile kauli rais aliitoa kama anamueleza kijana mdogo na au mwanaye!

Pili haipendezi kuanza kujenga malengo hasi na inaonyesha kuwa kuna mashaka fulani!

Rai yangu kwa rais; emb ajifikirie kuwa yeye angekuwa ndiye Meck Sadick kwa kauli ile angeipokeaje? Ndiyo maana vyuo vinafundisha communication skills! Ile CL111 pale thietre za UDSM hiyo ndiyo kazi yake! Uongee lipi ukiwa wapi na kwa nani!

Hizi kauli za kutishana kabla hata kazi haijaanza kwa kweli hazijengi! Zinazaa uoga na kutokujiamini! Magufuli atazame mfano wa mawaziri wake walivyokwama! Hii ni kutokana na uoga aliowajengea!
 
Kwahio kuambiwa 'ole wako uzitumie vibaya' ni kudhalilishwa na kutukanwa?

Wewe unaonaje?

Kama si wote, basi wengi wetu tunafanya chini ya usimamizi wa mtu flani (waweza kumwita boss au mkuu wako wa idara au supervisor au vyovyote)

Hebu suppose wewe na utu uzima wako unapewa maagizo na mkuu wako huyo kwa jina lolote kwa kutumia lugha kama ya huyu mkubwa, utajisikiaje?

Akutukanaye, hakuchagulii tusi mkubwa.....jiongeze!!
 
So ulitaka ambembeleze sio... kama ailvyokuwa akifanya baba MwanaAsha...

kwa taarifa tu... siku zake kama mkuu wa mkoa wa Dar znahesabika.
KWANI Umakini Na UKALI Ni KUPAYUKA Na Vitisho Tu!! VITENDO Vya Kiongozi Ndio Vinavyomtafsiri Ni Wa Aina Gani!! SIO Kupayuka Tu Hovyo!! MTAKATAA Hivi Sasa, Ila Muda Utafika Mtatafuta Machaka Ya Kuficha Sura Zenu!!! HII Nchi Imeoza Kinoma, Kutokana Na Mfumo Mbaya Wa Serikali Ya CCM! ABOMOE Mfumo Mzima, Sio Vitisho Tu!!! TOKEA Serikali Za Mitaa Na Magogoni Woote Baba Na Mama Mmoja Tu!!! JE, Hiyo Miaka 5 Atakuwa Anatisha Tu Watendaji Wake!!?
 
Hizi kauli ni sahihi kwa kipindi hiki cha mpito hakuna namna,kauli za ningeomba,nathani,ni vema mgeliona hili,zilitumika sana miaka 10 iliyopita hazijaleta matokeo chanya.
 
Umaarufu wa JPM umeongezeka kwa zaidi ya 20% na umaarufu wa huyo mwenzenu unaporomoka kwa kasi!
Kama ulidhani kwa mabandiko yenu haya ndio mtamshusha Mr. President basi hesabuni maumivu!!!
 
Nimesikia mara nyingi katika hotuba za Magufuli hakitoa heshima kwa wazee.Hatuwezi kujua kwa nini Magufuli hameamua kutoa kauli kama hiyo kwa Meck Sadick lakini tukiangalia matumizi ya funds zilizopita tunaweza kupata jibu.
 
Nadhani alikuwa anajaribu kutoa agizo juu ya kile kinachoonekana 'kuruhusu Dar es Salaam' kwenda kwa watu wa ovyo ovyo.
 
Badala ya kusema ole wako usitumie hizo pesa vibaya, angeweza kusema pesa itumike kwa matumizi yaliyokusudiwa. Ujumbe ni huo huo lakini ni namna ya kufikisha ujumbe kwa kutumia lugha tofauti.

Mimi sidhani kama kauli ililenga kumfedhehesha RC wa Dar. Zaidi ilikuwa inaakisi uozo uliopo katika matumizi ya fedha za serikali sehemu mbalimbali za nchi. Pamoja na yote hayo, JPM anayo nafasi ya kutumia lugha yenye staha zaidi bila kuathiri ujumbe wake kwa walengwa.
Tamko la "OLE wako" lina onyo ndaki yake.
Yaani kuna madahara mabaya kwako usipoyafuata maelekezo.
Na si agizo tu.
Hapa Kazi Tu.
 
Hakuna tatizo kabisa! baada ya kumtatulia tatizo, tena kwa ubunigu mkubwa ambao Meck Saddick hakufikiria, sasa kumweleza madhara ya iwapo fedha itatumika vibaya kuna ubaya gani? wewe ndo unakosea kwa sababu hukusikiliza vizuri, jitahidi usikilize kwa moyo wako wote, ni ajabu haujaona JPM alivotatua tatizo kwa ghafla.

Kama mtu anakurupuka kutatua matatizo basi huyo ndo anahitajika sasa!
 
Jana kwenye hotuba ya John Magufuli (rais wa Tanzania) alitumia kauli isiyo na weledi kutoka kwenye cheo alicho nacho kumueleza mtendaji wake ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadick! "Nitakupatia hizo fedha na OLE WAKO UZITUMIE VIBAYA" kauli ya "Ole wako uzitumie vibaya" ingawa hamtasema wala kuongea ila kiukweli ilimfedhehesha sana Meck Sadick!

Kwanza Meck Sadick kiumri ni mtu mzima sana kwa Magufuli! Lakini pia ni aina ya watu ambao wamestaharabika! Ile kauli rais aliitoa kama anamueleza kijana mdogo na au mwanaye!

Pili haipendezi kuanza kujenga malengo hasi na inaonyesha kuwa kuna mashaka fulani!

Rai yangu kwa rais; emb ajifikirie kuwa yeye angekuwa ndiye Meck Sadick kwa kauli ile angeipokeaje? Ndiyo maana vyuo vinafundisha communication skills! Ile CL111 pale thietre za UDSM hiyo ndiyo kazi yake! Uongee lipi ukiwa wapi na kwa nani!

Hizi kauli za kutishana kabla hata kazi haijaanza kwa kweli hazijengi! Zinazaa uoga na kutokujiamini! Magufuli atazame mfano wa mawaziri wake walivyokwama! Hii ni kutokana na uoga aliowajengea!
Mimi ni msukuma, baba yangu alivyokuwa anasoma canada Professor mmoja aliwahi mwambia ' I can get you out of the bush but I cannot get the bush out of you' magufuli ni msukuma typical....ubabe wa kisukuma...ni sawa na kuvaa suti na katambuga
 
Naona siku hizi watu wanakazi moja ktk hotuba ya Rais, ni kusikiliza neno kwa neno ili kuona Rais kakosea neno gani! Hivi karibuni yataanza hadi masahihisho ya spelling. Mngekuwa waandishi wa habari sipati picha hizo angle ambazo mngekuwa mnazipeleka news room!
Kwa kuwa hii ni habari, na kwa kuwa inaandikwa na watu, basi kila anayeandika habari ni mwandishi wa habari! Au unataka waandishi gani tena?
 
Hivi unashindwa kumuwajibisha mtu mkiwa wawili kwa staha mpaka uropoke barabarani???
That was a statement... Sikuona anamwajibisha mtu yoyote pale

Alitoa angalizo tu

Mkuu, muda wa kuremba umeisha... Tulikua tumezidi ujinga, wacha tu mkuu ajaribu mbinu nyingine
 
Back
Top Bottom