G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,598
- 36,027
Jana kwenye hotuba ya John Magufuli (rais wa Tanzania) alitumia kauli isiyo na weledi kutoka kwenye cheo alicho nacho kumueleza mtendaji wake ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadick! "Nitakupatia hizo fedha na OLE WAKO UZITUMIE VIBAYA" kauli ya "Ole wako uzitumie vibaya" ingawa hamtasema wala kuongea ila kiukweli ilimfedhehesha sana Meck Sadick!
Kwanza Meck Sadick kiumri ni mtu mzima sana kwa Magufuli! Lakini pia ni aina ya watu ambao wamestaharabika! Ile kauli rais aliitoa kama anamueleza kijana mdogo na au mwanaye!
Pili haipendezi kuanza kujenga malengo hasi na inaonyesha kuwa kuna mashaka fulani!
Rai yangu kwa rais; emb ajifikirie kuwa yeye angekuwa ndiye Meck Sadick kwa kauli ile angeipokeaje? Ndiyo maana vyuo vinafundisha communication skills! Ile CL111 pale thietre za UDSM hiyo ndiyo kazi yake! Uongee lipi ukiwa wapi na kwa nani!
Hizi kauli za kutishana kabla hata kazi haijaanza kwa kweli hazijengi! Zinazaa uoga na kutokujiamini! Magufuli atazame mfano wa mawaziri wake walivyokwama! Hii ni kutokana na uoga aliowajengea!