Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Aliyekuwa Mbunge wa Simanjiro kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ole Sendeka, amewataka Watanzania kuwapuuza watu wanaoeneza propaganda dhidi ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, akidai kuwa wengi wao ni wafanyabiashara waliokosa zabuni za Serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili, Oktoba 12, 2025 jijini Arusha, Sendeka amesema baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wakipata zabuni za kuendesha miradi ya Serikali kwa muda mrefu, hivi karibuni wamezikosa kulingana na sheria za manunuzi wamekuwa wakifadhili makundi ya vijana, vyombo vya habari visivyojiheshimu na wanaharakati wa nje ya nchi ili kuharibu taswira ya Serikali na ya chama tawala.
Amesema tabia hiyo imekuwa ikienezwa pia na baadhi ya wanachama wa CCM waliokosa uteuzi wa kugombea nafasi mbalimbali, ambao sasa wamegeuka kuendesha kampeni za kuwachafua walioteuliwa kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa ya habari.