Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,234
Mwanasiasa mkongwe na mbunge mstaafu wa jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka amesema kuwa chama cha mapinduzi hakiungi mkono mwenendo wa matukio ya utekaji yanayoripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Sendeka ameyasema hayo wakati akizunguma katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mkoani Arusha ambapo ameeleza kuwa matukio hayo yamekuwa yakirudisha nyuma ustawi wa amani na uhuru nchini.
"Kwanza utekaji ni jambo la hovyo, lifanywe na mtu binafsi, kundi watu, lifanywe na serikali ama lifanywe na mtu yoyote yule ni jambo la hovyo lisilozingatia misingi ya Utu. Hatukubaliani na utekaji wa aina yoyote, rai yangu kila mwnanchi aliye na habari kwamba kuna raia ametekwa na anamuhisi aliyemteka ni fulani ni vizuri watu wawe na ujasiri shida yetu wakati mwengine tunakuwa waoga, ni lazima ukubali kutoa gharama ya kutoa ushirikiano kwa vyombo ili huyo muhalifu aweze kukamatwa" amesisitiza Sendeka.