Ole Sendeka afichua ufisadi wa wabunge!

Ole Sendeka afichua ufisadi wa wabunge!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Bunge la Mchana siku ya Jumamosi wakati akihitimisha Hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mh Prof Muhongo alimuita Sendeka kuwa ni muongo kwa kutaka kumlisha Mh Rais Maneno ambayo hakuyasema.

Hii ni baada ya Mh Sendeka wakati akichangia hotuba hiyo alisema kua Rais hajatimiza Ahadi aliyowahi kutoa kuwa baada ya kuisha kwa Mkataba wa kampuni ya Tanzaniteone serikali itatwaa Mgodi huo na kumilikisha Wachimbaji wadogo wadogo. Migodi hiyo ipo Mererani wilayani Simanjiro mkoaniManyara.

Akimjibu Sendeka Mh Waziri alisema kua siku moja aliwahi kumuuliza swala hilo na yeye waziri alienda kwa Mh Rais na kumuuliza lakini Mh rais alisema kua hayo maneno hakuwahi kuzungumza isipo kua Sendeka anamsingizia.

Mh waziri alionya wale wote wenye tabia ya kuzungumza vitu vya uongo na kumlisha Rais maneno ambayo hakusema. Mh Waziri Muhongo Wakati akikamilisha kujibu hoja za Wabunge ndipo Mh Sendeka akaomba Muongozo lakini Spika alimkatalia.

Je Spika kumnyima Sendeka nafasi ya kuwasilisha Muongozo ni Demokrasia au anabalance mambo ili na wabunge wa Upinzani wakiomba muongozo awanyime kama tulivyoona?

MBUNGE wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, amewatuhumu baadhi ya wabunge na mawaziri kujihusisha na ufisadi wa kukwepa kodi kupitia utaratibu wa kuingiza sukari nchini.

Sendeka amewashawishi wabunge wenzake kumuunga mkono ili kujenga hoja ya kulishawishi Bunge kuunda kamati teule ya kuchunguza ufisadi uliopo katika uingizaji wa bidhaa hiyo.

Mbunge huyo alitoa tuhuma hizo juzi jioni wakati akichangia mjadala wa muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2013 uliowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, William Mgimwa.

"Mtakapochunguza nawahakikishieni humu ndani wengine watakosa mahali pa kuficha nyuso zao, maana ni wabia katika utaratibu huu," alisema.

Alisema kuwa utaratibu wa utoaji vibali kwa wafanyabiashara kuingiza sukari nchini ni lazima uangaliwe upya kwa wale wanaopewa, kwamba kuna mkakati wa kuwapa wakubwa wachache ambao ndio hao hao wenye ubia kwenye viwanda vya sukari.
"Wewe ndiye mwenye kiwanda cha sukari halafu unapewa kibali cha kuingiza sukari bila kulipa kodi. Kwa utaratibu huu viwanda vya ndani vitadorora na miwa ya wakulima wetu haitauzika," alisema.

Kwa sababu hao hao wanaohusika ndio wanadhibiti soko. Tukubali ‘monopoly' ya aina hii ni mbaya na hii haijalishi kama inafanywa na mwanachama wa CCM au wa chama chochote," alisema.

Alisema kama kuna kichaka kinachotumika kuiibia serikali sasa ni kupitia utaratibu huo wa uingizaji wa sukari na mchele nchini kwa kivuli cha kumsaidia mnyonge.

"Ndiyo maana leo sukari inayoingizwa nchini kwa utaratibu huo wa kutolipia kodi inauzwa kwa bei ile ile kama iliyoko kwenye soko ambayo imelipiwa kodi," alisema.



Source: Tanzania Daima
 
huyu mzee amenyimwa kitalu mererani ndio maana anatoa povu,wote wazee wa 10% hakuna msafi ccm
 
Siku hizi ni kawaida ku-balance equation! Ukiifungia Redio Imani, lazima uifungie pia Redio Kwa Neema! Ukisema Makanisa yanachomwa, ni lazima pia usema Msikitiki inachomwa-hata kama haujachomwa hata mmoja! CCM wakianza kuhubiri udini (CUF Waislamu, Chadema Wakatoliki), baadaye watasema waendesha udini ni CUF na Chadema- Hiyo yote ni ku-balance equation!!! This is Bongo!
 
Makinda amewekw pale kulinda maslahi ya ccm kwahiyo jambo lolote limaloweza kukiumbua chama au kumuumbua rais hawezi kuliacha lipite
 
JK kakataa kauli yake na Bi Kiroboto kamulinda kwa kutumia uspika wake, fungua hapa...

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...miliki-kampuni-ya-tanzanite-one-14-print.html

Halafu msome waziri wetu wa Nishati na Madini Mr muongo

DailyNews Online Edition - State to acquire 50 pc stake in TanzaniteOne

Kuthibitisha kuwa Sendeka anasema kweli basi soma hapa chini penye red...


Kweli Tanzania kuna wahuni, Mtu anaomba apatiwe kura na akishapata anachukua yeye kile alichowaahidi wapiga kura na kuvaa miwani ya mbao, Nafikiri James Ole Millya hapa ana siri ndefu
 
Siku hizi ni kawaida ku-balance equation! Ukiifungia Redio Imani, lazima uifungie pia Redio Kwa Neema! Ukisema Makanisa yanachomwa, ni lazima pia usema Msikitiki inachomwa-hata kama haujachomwa hata mmoja! CCM wakianza kuhubiri udini (CUF Waislamu, Chadema Wakatoliki), baadaye watasema waendesha udini ni CUF na Chadema- Hiyo yote ni ku-balance equation!!! This is Bongo!

Ni hakika mkuu kila kitu Serikali yetu "sikivu" inafanya kwa kubalance japokuwa Ndugu Musa Zungu aligoma sijui yeye ndo Msemaji wa Serikali.
 
Bunge la Mchana siku ya Jumamosi wakati akihitimisha Hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mh Prof Muhongo alimuita Sendeka kuwa ni muongo kwa kutaka kumlisha Mh Rais Maneno ambayo hakuyasema. Hii ni baada ya Mh Sendeka wakati akichangia hotuba hiyo alisema kua Rais hajatimiza Ahadi aliyowahi kutoa kuwa baada ya kuisha kwa Mkataba wa kampuni ya Tanzaniteone serikali itatwaa Mgodi huo na kumilikisha Wachimbaji wadogo wadogo.
Migodi hiyo ipo Mererani wilayani Simanjiro mkoaniManyara.

Akimjibu Sendeka Mh Waziri alisema kua siku moja aliwahi kumuuliza swala hilo na yeye waziri alienda kwa Mh Rais na kumuuliza lakini Mh rais alisema kua hayo maneno hakuwahi kuzungumza isipo kua Sendeka anamsingizia.
Mh waziri alionya wale wote wenye tabia ya kuzungumza vitu vya uongo na kumlisha Rais maneno ambayo hakusema.
Mh Waziri Muhongo Wakati akikamilisha kujibu hoja za Wabunge ndipo Mh Sendeka akaomba Muongozo lakini Spika alimkatalia.
Je Spika kumnyima Sendeka nafasi ya kuwasilisha Muongozo ni Demokrasia au anabalance mambo ili na wabunge wa Upinzani wakiomba muongozo awanyime kama tulivyoona?


Hapo kwenye red mkuu nia ya Spika sio Demokrasia wala kubalance mambo kuwaridhisha wapinzani hapa spika anajaribu kuifichia aibu serikali iwapo Ole Sendeka angekomaa kuleta ushahidi ili kudhibitisha kauli yake,ujue madam spika ana kazi mbili moja ni kuwadhibiti wapinzani na pili ni kuilinda serikali ya Dhaifu.
 
ah!!!!! nafuu Sendeka akasirishwe maana kasinzia sana. Na leo Dr. Slaa yupo Simanjiro, anamtafuna kwakwenda mbele.
 
WACHA MOTO UWAKE, :A S-fire1: SERIKALI INAKOPA HELA WORLD BANK NA ADB DOLLA MILLION 500 KULIPIA MADENI YA TANESCO, NI UPUUUZI WA HALI YA JUU, PROFESA BORA AKASHIKE CHAKI
 
Ile hutuba ilikuwa na magumashi kibao! Inaonekana alichokuwa akikiongea wazir hakina fact yeyote kakosea saaana ... Kajichanganya mpaka akasema walishajiloga wakauza nchi(sehemu zote za machimbo) so kama walivo impotence hawana uwezo wa kujisahahisha ili kuwapa wananchi japo kasemu kakuchimba ile hali kila siku utawasikia wakituhadaa kuwa mikataba yote mibovu wanaipitia upya kumbe danganya toto kama hii aliyofanyiwa olesendeka!!
 
Hata akileta ushahidi utafungiwa kabatini tu. bongoo!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Naamini JK ahadi alizo toa wakati wa kampeni anaweza akawa anakumbuka kumi tu.
 
Bunge la Mchana siku ya Jumamosi wakati akihitimisha Hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mh Prof Muhongo alimuita Sendeka kuwa ni muongo kwa kutaka kumlisha Mh Rais Maneno ambayo hakuyasema. Hii ni baada ya Mh Sendeka wakati akichangia hotuba hiyo alisema kua Rais hajatimiza Ahadi aliyowahi kutoa kuwa baada ya kuisha kwa Mkataba wa kampuni ya Tanzaniteone serikali itatwaa Mgodi huo na kumilikisha Wachimbaji wadogo wadogo.Migodi hiyo ipo Mererani wilayani Simanjiro mkoaniManyara.Akimjibu Sendeka Mh Waziri alisema kua siku moja aliwahi kumuuliza swala hilo na yeye waziri alienda kwa Mh Rais na kumuuliza lakini Mh rais alisema kua hayo maneno hakuwahi kuzungumza isipo kua Sendeka anamsingizia.Mh waziri alionya wale wote wenye tabia ya kuzungumza vitu vya uongo na kumlisha Rais maneno ambayo hakusema. Mh Waziri Muhongo Wakati akikamilisha kujibu hoja za Wabunge ndipo Mh Sendeka akaomba Muongozo lakini Spika alimkatalia.Je Spika kumnyima Sendeka nafasi ya kuwasilisha Muongozo ni Demokrasia au anabalance mambo ili na wabunge wa Upinzani wakiomba muongozo awanyime kama tulivyoona?
Hapana, Spika alikuwa akimlinda Rais na ahadi yake, maana angemruhusu angethibitisha kuwa hajatendewa haki kuitwa muongo.
 
Back
Top Bottom