Ole Sendeka afichua ufisadi wa wabunge!

Ole Sendeka afichua ufisadi wa wabunge!

Bunge la Mchana siku ya Jumamosi wakati akihitimisha Hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini mh Prof Muhongo alimuita Sendeka kuwa ni muongo kwa kutaka kumlisha Mh Rais Maneno ambayo hakuyasema. Hii ni baada ya Mh Sendeka wakati akichangia hotuba hiyo alisema kua Rais hajatimiza Ahadi aliyowahi kutoa kuwa baada ya kuisha kwa Mkataba wa kampuni ya Tanzaniteone serikali itatwaa Mgodi huo na kumilikisha Wachimbaji wadogo wadogo.
Migodi hiyo ipo Mererani wilayani Simanjiro mkoaniManyara.

Akimjibu Sendeka Mh Waziri alisema kua siku moja aliwahi kumuuliza swala hilo na yeye waziri alienda kwa Mh Rais na kumuuliza lakini Mh rais alisema kua hayo maneno hakuwahi kuzungumza isipo kua Sendeka anamsingizia.
Mh waziri alionya wale wote wenye tabia ya kuzungumza vitu vya uongo na kumlisha Rais maneno ambayo hakusema.
Mh Waziri Muhongo Wakati akikamilisha kujibu hoja za Wabunge ndipo Mh Sendeka akaomba Muongozo lakini Spika alimkatalia.
Je Spika kumnyima Sendeka nafasi ya kuwasilisha Muongozo ni Demokrasia au anabalance mambo ili na wabunge wa Upinzani wakiomba muongozo awanyime kama tulivyoona?

Sendeka ni mnafiki sssana, kama Sitta tu na Kilango....walijifanya wapapmbanaji wa ufisadi wakawapaka matope kina kina Lowassa..then anajidai kujirudi ...wenzie bado wanakinyongo sana nae!!!
Wamemkomesha!!
 
MBUNGE wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, amewatuhumu baadhi ya wabunge na mawaziri kujihusisha na ufisadi wa kukwepa kodi kupitia utaratibu wa kuingiza sukari nchini.

Sendeka amewashawishi wabunge wenzake kumuunga mkono ili kujenga hoja ya kulishawishi Bunge kuunda kamati teule ya kuchunguza ufisadi uliopo katika uingizaji wa bidhaa hiyo.

Mbunge huyo alitoa tuhuma hizo juzi jioni wakati akichangia mjadala wa muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2013 uliowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, William Mgimwa.

"Mtakapochunguza nawahakikishieni humu ndani wengine watakosa mahali pa kuficha nyuso zao, maana ni wabia katika utaratibu huu," alisema.

Alisema kuwa utaratibu wa utoaji vibali kwa wafanyabiashara kuingiza sukari nchini ni lazima uangaliwe upya kwa wale wanaopewa, kwamba kuna mkakati wa kuwapa wakubwa wachache ambao ndio hao hao wenye ubia kwenye viwanda vya sukari.
"Wewe ndiye mwenye kiwanda cha sukari halafu unapewa kibali cha kuingiza sukari bila kulipa kodi. Kwa utaratibu huu viwanda vya ndani vitadorora na miwa ya wakulima wetu haitauzika," alisema.

Kwa sababu hao hao wanaohusika ndio wanadhibiti soko. Tukubali ‘monopoly' ya aina hii ni mbaya na hii haijalishi kama inafanywa na mwanachama wa CCM au wa chama chochote," alisema.

Alisema kama kuna kichaka kinachotumika kuiibia serikali sasa ni kupitia utaratibu huo wa uingizaji wa sukari na mchele nchini kwa kivuli cha kumsaidia mnyonge.

"Ndiyo maana leo sukari inayoingizwa nchini kwa utaratibu huo wa kutolipia kodi inauzwa kwa bei ile ile kama iliyoko kwenye soko ambayo imelipiwa kodi," alisema.



Source: Tanzania Daima
 
sendeka nalo jizi.
hile kauli yake ya "serikali sikivu ya chama cha mapinduzi"huwa ni kujisahau au kutokujua anachosema au ni unafiki,
haya majitu kweli ni janga kwa taifa.
Sendeka nae mwizi tu hana lolote huyo..kua sisiemu ni sawa na kuwa kwenye jela ya fikira huru,uhuru wa kufikiri.
 
Nakuu mkono mkuu ni kweli kabisa ulichosema ila ya mwisho.
[/COLOR]
Hapo kwenye red mkuu nia ya Spika sio Demokrasia wala kubalance mambo kuwaridhisha wapinzani hapa spika anajaribu kuifichia aibu serikali iwapo Ole Sendeka angekomaa kuleta ushahidi ili kudhibitisha kauli yake,ujue madam spika ana kazi mbili moja ni kuwadhibiti wapinzani na pili ni kuilinda serikali ya Dhaifu.
 
Back
Top Bottom