Ole Sendeka aeleza siri ya ukimya wake bungeni

Mirerani. Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amesema kwa sasa hazungumzi sana Bungeni kutokana na utendaji kazi mzuri wa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Ole Sendeka akizungumza na wadau wa madini ya Tanzanite, mji mdogo wa Mirerani, amesema amekuwa kimya Bungeni kwani hivi sasa viongozi wa serikali wanaofanyia kazi changamoto za wananchi.

Amesema kipindi chake cha miaka 10 ya ubunge wake alikuwa anazungumza mara nyingi Bungeni kwa sababu baadhi ya mambo hayakuwa sawa.

Amesema kila changamoto ya wapiga kura wake inapojitokeza viongozi wa serikali wanaifanyia kazi hivyo anakosa sababu ya kuzungumza.

"Wadau wa madini walipokuwa wanapekuliwa bila staha nilifikisha kilio hicho Serikali na sasa hivi wanapekuliwa kwa staha," amesema Ole Sendeka.

Amesema akiwa na jambo mkuu wa mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere anatatua, likihusu Simanjiro, mkuu wa wilaya hiyo Dk Suleiman Serera anafanyia kazi hivyo hana sababu ya kulalamika.
Viongozi wetu kwa Unafiki tumewazoea yule mwingine anasema Watanzania wamemwambia hawataki Katiba Eti Wanataka Maendeleo hao Watanzania alikutana nao wapi mbona yeye Mwenyewe Alishuriki Bunge la KATIBA akala na POSHO
 
Mkuuu hiki chama ndio kinatusababishiaa umaskin mkubwa sana na dhiki chama hakina muelekeo mpya kila cku upuuz ule ule
Na ndiyo hawa hawa wanao tutaka eti tuhamie Burundi iwapo tutashindwa kulipa kodi zao kandamizi. Yaani wameigeuza hii nchi kuwa mali yao na vizazi vyao.

We ngoja tu! Ipo siku tutaamka tu kutoka usingizini.
 
Kabisa Mkuu ndiyo sababu hawa wahuni wanahaha sasa na huyo Simbachawene anatafuta namna ya kudhibiti Twitter Space na hasa ya Maria ambayo kwa nyakati mbali mbali imevuta wasikilizaji hadi karibu 7,000 kwa siku moja.

Hakuna jinsi ya kuzuia hii kitu ila nina wasiwasi mkubwa na usalama wa Maria hasa ukitilia maanani wasiojulikana wamemaliza likizo zao na wamerudi rasmi kazini.
Very sad,Watu wasiojulikana hawakuwa likizo, wakienda mafunzoni, Sasa wanakuja wakiwa hatari zaidi
 
Kila siku viongozi ni watoto wao tu sie watoto wa watu ukisoma sana nafasi kuwa umekuwa Doctor ova ma naibu na ma waziri ni watoto wao tu ila kuna siku tutaelewana tu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom