tang'ana
JF-Expert Member
- Apr 3, 2015
- 11,809
- 15,055
Mirerani. Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka amesema kwa sasa hazungumzi sana Bungeni kutokana na utendaji kazi mzuri wa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Ole Sendeka akizungumza na wadau wa madini ya Tanzanite, mji mdogo wa Mirerani, amesema amekuwa kimya Bungeni kwani hivi sasa viongozi wa serikali wanaofanyia kazi changamoto za wananchi.
Amesema kipindi chake cha miaka 10 ya ubunge wake alikuwa anazungumza mara nyingi Bungeni kwa sababu baadhi ya mambo hayakuwa sawa.
Amesema kila changamoto ya wapiga kura wake inapojitokeza viongozi wa serikali wanaifanyia kazi hivyo anakosa sababu ya kuzungumza.
"Wadau wa madini walipokuwa wanapekuliwa bila staha nilifikisha kilio hicho Serikali na sasa hivi wanapekuliwa kwa staha," amesema Ole Sendeka.
Amesema akiwa na jambo mkuu wa mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere anatatua, likihusu Simanjiro, mkuu wa wilaya hiyo Dk Suleiman Serera anafanyia kazi hivyo hana sababu ya kulalamika.