Uchaguzi 2020 Ole Sabaya awaongoza Wananchi wa Hai kumsindikiza Magufuli kwa Mbio

Baada ya Mkutano Mkubwa ukiofanyika BOMANG'OMBE Jimboni Hai Wananchi wameamua kuusindikiza msafara wa Rais Magufuli kwa kukimbia Mbio ili kuonesha mapenzi yao kwake na ccm . Video inamuonesha Dc Ole Sabaya akiongoza Wananchi hao

Pamoja na Upinzani kupeleka viongozi wote Jimboni Hai lakini wamegonga Mwamba maana Wananchi wamejitokeza kwa wingi leo WAKIWA wamebeba majani aina ya masare kuonesha kuomba Radhi kwa kumchagua Mbowe ambae amekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya Hai.

Wachaga wa siku hizi wasanii sana. Wana utani na masare.
Askofu Shoo ngoja akienda huko....
 
Kwi kwi kwi! Yaani mbio za maandamano ya Hai zinapishana na wachaga wanaojiendea zao mashambani hata habari hawana?
Upoloto was kiwango cha dilimulaina
 
Kwa hiyo hio ndo nyomi iliyomsindikiza magufuli akiondoka hai???!! Daah
Itakuwa wananchi waliomsindikiza Lissu Mwanza hadi hotelini usiku waliwaumiza sana roho ndugu zangu wa mboga mboga.

Nani mwenye ile video atukumbushe jamani, Sabaya aelekezwe namna umati unavyopaswa kumsindikiza mgombea
 
Majani wanayabeba wakiomba msamaha mambo ya ugomvi yaishe
Ok hayaitwi masare ni masale na pia kazi yake sio hiyo uliyoitaja sababu sio kila msamaha anaombwa na hayo majani.

Sale ni jani la heshma na linabeba mambo mengi makubwa na ya kimila uchagani. Kushika sale wakati kiongozi au chief/mangi anapita ni heshma kubwa sana kwake. Kwa Yale masale ya jana ni wazi rais John Pombe Magufuli amepokelewa kwa heshma ya mangi/mfalme kwenye ardhi ya wachaga

Sale linaweza kutumika kuomba msamaha kwa makosa makubwa sana ambayo yameshindikana kutatuliwa na wakubwa wowote. Hapo ndio mkosaji anaweza kupewa ushauri na wazee achukue Hilo jani tena sio jani ilimradi... kuna sehemu yoyote maalum na uchumaji wake kama ni kwaajili ya msamaha
 
Daaa huu ukoro sana hii nchi ina wasanii wengi sana yani basi tu japo sikitika kuona ujinga ndiyo unaendesha nchi. Mungu anisame sana maana sitaki kuona ccm maanayake watu wake sasa watu wako wamefetuka yani hii kujimwa elimu ndiyo madhara yote haya,japo tumetoka mbali sana hivi kipindi wambunge walikuwa wa ccm eti hamuendi madarasani unamsubiria ubunge na wananchi hukaa barabarani daaa hongereni sana wapinzani.
 
Nje ya mada. Jee Leo Janeth Magufuli alimsindikiza mume wake kwenye kampeni Kilimanjaro?
 
Ok hayaitwi masare ni masale na pia kazi yake sio hiyo uliyoitaja sababu sio kila msamaha anaombwa na hayo majani.

Sale ni jani la heshma na linabeba mambo mengi makubwa na ya kimila uchagani. Kushika sale wakati kiongozi au chief/mangi anapita ni heshma kubwa sana kwake. Kwa Yale masale ya jana ni wazi rais John Pombe Magufuli amepokelewa kwa heshma ya mangi/mfalme kwenye ardhi ya wachaga

Sale linaweza kutumika kuomba msamaha kwa makosa makubwa sana ambayo yameshindikana kutatuliwa na wakubwa wowote. Hapo ndio mkosaji anaweza kupewa ushauri na wazee achukue Hilo jani tena sio jani ilimradi... kuna sehemu yoyote maalum na uchumaji wake kama ni kwaajili ya msamaha

Kwahiyo siku hizi mnayabeba baba tu? Unajua kama nisingekuwa na kihamba nisingeelewa ninachosema
 
Kwahiyo siku hizi mnayabeba baba tu? Unajua kama nisingekuwa na kihamba nisingeelewa ninachosema
Kwa Yale masale ya jana ni wazi rais John Pombe Magufuli amepokelewa kwa heshma ya mangi/mfalme kwenye ardhi ya wachaga na amepewa heshma kubwa na baraka kuongoza nchi
 
Kwa Yale masale ya jana ni wazi rais John Pombe Magufuli amepokelewa kwa heshma ya mangi/mfalme kwenye ardhi ya wachaga na amepewa heshma kubwa na baraka kuongoza nchi
Indeed. Ila wasije wakaenda tena na masàle kwa mwingine. We are living in the world, full of confusion
 
Hahaahaahaha. Kama Ni hivyo Basi siutaki ukuu wa Wilaya Wala mkoa chini ya uongozi wa Magufuli
kwenye siasa inabidi uwe mnafiki na mtu wa kujipendekeza all in all chagua magufuli mkuu mitano tena
 
Indeed. Ila wasije wakaenda tena na masàle kwa mwingine. We are living in the world, full of confusion

Imepita hiyo

Sikuyaona Kwa Tundu wala maalim seif.

Siasa za mkoa wa Kilimanjaro zinahitaji uelewa mkubwa sana, wakongwe wa siasa kina Zakhia Megji wanaelewa😀😀
 
Zilikuwa zama za ujinga nazo zimepita anajutia sasa mungu kwake amemwacha
 
Back
Top Bottom