Ole Mushi: Yanga imepiga kwenye mshono

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Na Thadei Ole Mushi.

1. Pale Simba kwa wachezaji wa Nje wabaki wawili tu Inonga na Kanoute. Hawa kina Onyango ni wakati wa kwenda kupiga kura huko Kenya na Kubakia huko huko.

2. Mayele hakufunga lakini kwangu huyu ndiye man of the Match. Jamaa kakichafua sana na kathibitisha kuwa Onyango anastahili kustaafu kwa Heshima.

3. Makambo Mashabiki wanampenda sana lakini Miguu yake imemkataa. Huyu atafute timu mapema anapaswa kuachwa.

4. Wakati Pablo anakuja nilisema kuwa Simba walihitaji wachezaji bora kwanza kabla ya kumtafuta Kocha mzuri. Walitukana lakini kwa kikosi kile hata aje Gurdiola hawezi kubadili matokeo.

5. Yanga haipaswi kubweteka kuna maeneo ya Kufanyia kazi hasa Beki wa Kushoto. Yupo kibwana anajitahidi sana japokuwa kiasili si beki wa Kushoto kuumia kwake leo kama Kibu angeendelea na ubora alikuwa nao na hakuumia wangesawazisha.

6. Yanga imepiga kwenye Mshono... Match hii imewauma sana Watani ni bora wangefungwa na Yanga kwenye ligi kuu lakini si kuwaondoa kwenye kombe la Azam. Ni mahali Pekee ambapo palikuwa pamebakia pa kuambulia chochote msimu huu.

7. Simba ina kazi kubwa ya kukisuka upya Kikosi chao. Kusuka kikosi cha Kupata ushindi inahitaji muda sana. Mpaka waje kupata combination kama ya Chama na Mickson sio leo wala Kesho. Si mara zote usajili unaweza kukulipa ni bahati nasibu kwenye kua assemble timu. Hili limewakuta Yanga miaka minne nyuma wamenunua wachezaji na kuachana nao kwa kuwa hawakutoa kilichotarajiwa.

8. Simba wamejifunza kuwa Mpira sio pesa tu.... kitendo cha kuwauz key players wao (Chama na Mickson) wasije kukirudia tena kama hawana mbadala.

9. Manara anabakia kuwa mtu mwenye furaha zaidi msimu huu, Kahama na Vikombe vyake pale Simba kama yanga itafanikiwa kuchukua ubingwa katika mashindano yote. Jamaa ana kismart flan hivi. Kila anachokishika kwenye Soka kinamlipa..... amekuja Yanga ikiwa ya Kawaida kabisa.... katujengea kujiamini. MANARA ana Mchango mkubwa sana pale Yanga.

10. Feisal Salum Abdalah.... Maeneo kama yake hakuachi. Kamwadhibu sana Kakolanya.... amehatarisha pia afya yake na Mkataba wake. Sina Kumbukumbu sahihi kama hawa wawili waliwahi kugombana...

Ukichukia Uwe na Sababu na Ukifurahi Share.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Na wewe umepiga tena muremure kwenye mushono mura.
 
Uchambuzi mzuri

Kwa kuongezea tu simba tatizo liko kwenye menejimenti. Haijawa sawa kiuongozi

Halafu tatizo serious zaidi menejiment ndo inatafuta wachezaji bila mapendekezo ya kocha.

Pale yanga, Eng. Herz anasajiri waliopendekezwa na kocha tu. Wote wa nje na wandani ni mapendekezo ya kocha. Ni makambo pekee alirudishwa kwa ushawishi wa mashabiki
 
Hiyo namba 9 nitakataa mpaka kesho. Manara hana impact yoyote ile Yanga! Usajili mzuri na benchi zuri la ufundi, vimefanywa na GSM! Nadhani pongezi nyingi zingeenda huko.

Huko kwingine walau kuna uhalisia.
Nadhani hujamuelewa jamaa vizuri, katika mpira wetu wa kibongobongo lazima kuwe na mtu wa propaganda, achana na hii kitu ni hatari sana kwa adui yako na Manara amejaaliwa hicho kitu.
 
Hiyo namba 9 nitakataa mpaka kesho. Manara hana impact yoyote ile Yanga! Usajili mzuri na benchi zuri la ufundi, vimefanywa na GSM! Nadhani pongezi nyingi zingeenda huko.

Huko kwingine kuna uhalisia.
Manara ni albino . Hata GSM kumtafuta Manara kwa hudi na uvumba wanajua wanachokifanya. Manara ataifanya Yanga ibebe ubingwa wa Dunia ngazi ya vilabu.Sisi Mashabiki kindakindaki wa Yanga tunaamini hivyo , we endelea na dharau zako za kumdharau Manara .
 
Mimi namdharau kwa sababu tu ya mchango wake mdogo tangu alipohamia Yanga. Na siyo kwa sababu ya Ualbino wake.
 
Yaani timu iliyoshinda ni bora sana na iliyofungwa ni dhaifu sana ila timu bora imeshindwa kuifunga timu dhaifu japo goli 3
Simba ni bora sana nenda CAF rankings watakupa majibu
 
Timu bora hucheza kwa malengo (objectively). Haiwezi kuhatarisha utimamu wake kwa mechi muhimu zinazofuata kwa kulazimisha mabao zaidi kwa nia ya kumkomoa mpinzani tu, wakati hata nusu goli linatosha kuivusha. Hoja yako ingekuwa sahihi zaidi iwapo Yanga ilitakiwa lazima ipate mabao matatu ndiyo isonge mbele. Vigezo vya CAF ni subjective, siyo objective. Yaani si lazima kila mtu akubaliane navyo kwa sababu havikuegemezwa kwenye vipimo vinavyokubalika na kila mtu. Mathalan, kwangu mimi kipimo cha ubora wa timu lazima kiweke muda uliotumika kupima ubora huo. Mwaka mmoja, mitatno, muda wote? Kama ni ubora wa muda wote, basi Simba ili iwe ya kumi, mathalan, lazima iwe miongoni mwa timu kumi zilizowasilishwa kubeba ubingwa wowote ule wa Afrika kwa muda wote. Kama ni ubora wa mwaka mmoja, basi usitajwe kama vile ni ubora wa muda wote. Na anayejisifia awe anajua ni kwa vigezo vipi na vimepatikanaje: utajiri? Wingi wa wanachama? maoni ya wapiga kura? miundombinu ya klabu? Awe anajua maana na tafsiri ya ngazi za ubora. Awe anajua kwamba si lazima vigezo vya urembo vya Miss Tanzania viwe ndiyo vifuatwe na kijana anayetafuta mchumba. La sivyo dunia hiyohiyo moja ingekuwa na mrembo mmoja tu kila mwaka badala ya kuwa na Miss World, Miss Universe, Miss International, Miss Earth. Na Ulaya hiyohiyo moja isingekuwa na wachezaji bora tofauti kwa bara hilohilo moja, UEFA footballer of the year, Ballon d’Or, n.k. Kwa hivyo vigezo vya CAF siyo lazima viwe ndiyo vigezo visivyopingika vya ubora wa timu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom