Ole Millya kuvuliwa uanachama CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ole Millya kuvuliwa uanachama CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by nngu007, Jun 8, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Said Njuki, Arusha

  MGOGORO ndani ya CCM Mkoa wa Arusha umeshika kasi mpya baada ya Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati ya Siasa za chama hicho mkoa kudaiwa kumvua
  uanachama Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) Mkoa, Bw. James Ole Millya.

  Pia vijana wengine watano wa umoja huo wanaodaiwa kuwa vinara wa mgogoro nao watakumbwa na rungu hilo baada ya kamati hizo kutoa mapendekezo ya kufukuzwa uanachama kwa kitendo chao cha kushadadia kuondoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Bi. Mary Chatanda.

  Habari kutoka ndani ya vikao hivyo ambazo zimethibithswa na baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa sharti la kutotajwa majina, zimedai Kamati hiyo iliyoketi mwishoni mwa
  wiki ilitoa mapendekezo yake kuwa Mwenyekiti huyo anayedaiwa kuwa kinara wa mgogoro huo pamoja na vijana hao avuliwe madaraka.

  Vyanzo hivyo vilidai kuwa kikao cha kamati hiyo pia kilihudhuriwa pia na wajumbe kutoka Kamati ya Maadili ya Taifa ikiongozwa na Kanali Mhando na wajumbe wawili kutoka UVCCM Taifa ambao ni Bw. Seif Malinda na Mzee Mipoko kilichokaa kuanzia asubuhi hadi usiku wa manane.

  Mapendekezo hayo baada ya kuridhiwa na wajumbe hao yalifikishwa katika Kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa, kilichofanyika siku moja baadaye na kuridhia mapendekezo hayo, hivyo kusubiri kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kinachotarajiwa kukutana Jumamosi wiki hii kwa ajili ya maamuzi zaidi.

  Vyanzo hivyo vimewataja majina ya vijana watano kati ya 11 waliohojiwa siku hiyo, kufuatina mgogoro unaotokana na falsafa mpya ya CCM ya kujivua gamba ambapo makada waandamizi wa chama hicho, aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge wanashinikizwa kuachia ngazi zao.

  Baadhi ya sababu zilizoelezwa za kuwajibika kwa Bw. Milly
  Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Bi. Mary Chatanda.

  Wadadisi wa mambo ya siasa mkoani hapa wameeleza ya kuwa iwapo hatua hiyo ya kuwavua uwanachama vijana hao itatekelezwa itazidi kuchochea na kupanua mgogoro huo ambao ungeweza kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia na kupunguza ufa ndani ya chama hicho.

  Lakini kundi lingine linatoa matamshi mazito dhidi ya makada hao na kueleza kuwa wanapaswa kuwajibika kwa tuhuma zinazowakabili na kwenda mbali zaidi na kumtaja Bi. Chatanda ni lulu ya chama mkoani hapa na hapaswi kuondoka.
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wacha wafu wazike wafu wenzao.
   
 3. v

  van victor Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakishapambana wao kwa wao kazi kwetu chadema itakuwa rahisi....
   
 4. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Vita hiyo ni sawa na vita ya wachawi wanaouliana watoto.
  Let them kill each other
   
 5. l

  lemberwa Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani hiyo safi sana wanatupa nafasi sisi chadema kazi rahisi ya kulichukua jiji letu milele
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Dhambi ya kuua inawala.
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Wamalizane
   
 8. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mambo ya uvccm chatanda na uvccm millya hayo
   
 9. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  kumuondoa millya ni ndoto ya mchana hawawezi ana mizizi mirefu saaana hebu jiulizeni alipataje huo uenyekiti afu ndo tujadili mengine
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  madhara ya siasa topetope
   
 11. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Huyo ole millya ndio aliwazuia kuchukua jiji?
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tusubiri na kuona kitakachotokea!!!
   
 13. M

  Makupa JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  cdm jiandaeni kumpokea kama kawaida yenu
   
 14. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,450
  Likes Received: 782
  Trophy Points: 280
  Sio habari
   
 15. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,303
  Likes Received: 973
  Trophy Points: 280
  Vita vya Panzi.
   
 16. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  cdm chama makini, anakaribishwa sharti atubu dhambi zake na asitegemee kupewa cheo chochote. Akubali kuwatumikia watz na sio mtu kama anavyofanya huko kwenye magamba. Uko hapo? Umeridhika? Kachukue ujira wako kwa leo, tuonane kesho tena.
   
 17. J

  John W. Mlacha Verified User

  #17
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  kaamua ajiondokee mwenyewe ..mchawi wanamjua wenyewe
   
 18. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #18
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  kumbe sakata lilianza zamani?
   
Loading...