Old Is Gold

Dengue

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
2,050
Reaction score
1,470
Wale wa zamani hii kitu inaitwaje?
 

Attachments

  • 1392138994712.jpg
    23.2 KB · Views: 296
Shati hilo likiitwa slimfit.

Suruali hizo zikiitwa, Pecos au Bellbottom, au Bugaluu.

Viatu hivyo vikiitwa, mkuki moyoni au spearman.

Na huyo mtu akiitwa, chale.
 
Shati hilo likiitwa slimfit.

Suruali hizo zikiitwa, Pecos au Bellbottom, au Bugaluu.

Viatu hivyo vikiitwa, mkuki moyoni au spearman.

Na huyo mtu akiitwa, chale.

Duh ya kweli ni dhahabu.
 
Shati hilo likiitwa slimfit.

Suruali hizo zikiitwa, Pecos au Bellbottom, au Bugaluu.

Viatu hivyo vikiitwa, mkuki moyoni au spearman.

Na huyo mtu akiitwa, chale.

we oldtimer!!!-macheckbob wa enzi zenu uko kigoli ...
 
Wale wa zamani hii kitu inaitwaje?

Hyo kakosea vitu viwili au vitatu, nguo hizo zilkuwa hazivaliwi na viatu hivyo, zilikuwa zinavaliwa na viatau vinaitwa "rise-on" Na nguo hizo zilikuwa hazivaliwi na tai hizo, zilikuwa zinavaliwa na kitu kama scarf hivi. Na kofia aina ya Marvin Gaye.


 

Kumbe ni rise on hii laison ni kurahisisha tu matamshi.
 
Shati hilo likiitwa slimfit.

Suruali hizo zikiitwa, Pecos au Bellbottom, au Bugaluu.

Viatu hivyo vikiitwa, mkuki moyoni au spearman.

Na huyo mtu akiitwa, chale.

Na style ya nywele je?
 
Halafu huyu jamaa anaonesha ni Chadema
 
Duh enzi hizo itakua hair relaxer zilikua hazijaanza kutumiwa siku hizi kila mtu ana singa lol

Enzi hizo watakao singa inabidi wazichome, eeh mama watu waliungua vichwa kwetu hapa, kwa kupiga nywele pasi zinyooke. Kitana la chuma kubwa utafikiri zile nyundo za mafundi risasi, linawekwa kwenye jiko la moto, likipata moto ndio linawekwa kichwani kupiga pasi nywele, akikosea kidogo kaunguza kichwa. La haula, yote kutaka singa.
 
Shati hilo likiitwa slimfit.

Suruali hizo zikiitwa, Pecos au Bellbottom, au Bugaluu.

Viatu hivyo vikiitwa, mkuki moyoni au spearman.

Na huyo mtu akiitwa, chale.

Duh, we noma. Na tai inaitwaje?
 
Duh, we noma. Na tai inaitwaje?

Tai ikiitwa tai. Lakini nani avae tai enzi hizo, cheza na Nyerere? Ukivaa tai unaambiwa bepari siku ya pili lazima uje kusachiwa nyumbani kwako.

Tai watu wakivaa wakienda kujirusha na dinner Kilimanjaro Hotel, Simba Grill, hapo wanaume walikuwa hawaingii bila tai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…