Yeah, that's nice analogue. Anachosisitiza Bin Kleb ndicho hicho hicho alichokuwa anasisitiza Frederic Kitengie, GM wa Mazembe, lakini ukweli ukajulikana......but a Mazembe official insisted the Bokungu transfer was legal
...Alipoulizwa kuhusu utata wa sakata lake ambalo limefika hadi FIFA, Kleb alisema; "Tumefuatilia kote, hadi kwa wanasheria, na tumefanikiwa kupata hadi ITC yake, nawaambia mashabiki wa Yanga wajue viongozi wao wanafanya kazi, hatuna stori nyingi, sisi tunafanya vitendo, tunafanya kazi kwa siri sana,".
"Na tumepitia sehemu zote, tumeona kabisa tuko sahihi katika kumsajili mchezaji huyu na hakutakuwa na tatizo lolote upande wetu,"alisema.
Kuelewa hii unahitaji uwe tayari unajua series ya usajili wa Okwi kutoka Simba => Etoile => SC Villa => Yanga, halafu uwe na kumbukumbu ya jinsi TP Mazembe ilivyonyang'anywa ushindi kwa kumtumia mchezaji waliyeuziwa na kuidhinishwa na chama cha soka kingine (FECOFA - DRC) tofauti na kile ambacho mchezaji huyo ana mkataba na klabu iliyo chini yake (FTF - Tunisia)Bado sijaelewa kabisa
Bado sijaelewa kabisa
Hii imekula kwao Yeboyebo
Mkuu, sakata la Mazembe lilitokea 2011 huku TMS ilikuwa tayari imeshaanza tangu 1st October 2010. Katika hili, vilabu husika vinavyouziana mchezaji vikikamilisha kuingiza information zao kwenye TMS, ndipo chama cha soka cha nchi anakotoka mchezaji kinatuma ITC kwa chama anachoenda mchezaji. Ishu ya Bokungu ni kwamba Mazembe waliidharau timu yake halisi ya Esperance ambayo ndiyo ilikuwa ina mkataba naye, badala yake wakamnunua kutoka Virunga ambayo nako alikuwa anaichezea kimakosa. Kwa hiyo utagundua kuwa chama cha soka cha DRC kilifanya makosa kumuidhinisha kienyeji bila kujaza TMS na kupewa ITC, lakini bado huo haukutosha kuwa utetezi wa Mazembe kutonyang'anywa point kwani ilikuja kuonekana na CAF kwenye system kwamba alitakiwa afanyiwe uhamisho kutoka Esperance, na sio Virunga. Hivyo hivyo Okwi anatakiwa afanyiwe uhamisho kutoka Etoile, na sio SC Villa. Kwa hiyo TFF inaweza kumuidhinisha kienyeji Okwi acheze Yanga, lakini pale timu yoyote itakapolalamika CAF au FIFA, itakuja kugundulika kwamba vilabu vilivyotakiwa kujaza information kwenye TMS ni Etoile na Yanga, ambapo baada ya information ku-match, chama cha soka cha Tunisia (FTF) kingeituma ITC kwenda chama cha soka cha Tanzania (TFF), jambo ambalo halijafanyika!...
2. Wakati ule hakukuwa na utaratibu wa Matching Transfer System, na kwa hivyo aibu ya pointi za mezani kwa kasoro za usajili ilikuwa bado ikiiandama CAF. Tangu kuanza kwa utaratibu huo, uwezekano wa mchezaji kuhamishwa isivyo halali haipo.
hoja ya msingi hapa ni iwapo TMS ilikwishaanza kutumika, na kama ndio, ilitumika ipasavyo. Sifa mojawapo ya mtandao (network) ni kufananisha takwimu zinazoingizwa na zilioko kwenye database. Kwa hivyo hata kama Villa itaingiza taarifa kuwa Okwi ni mchezaji wake halali, database ya CAF lazima itabaini iwapo ni halali kweli au la. Na huo ndio uzuri wa TMS. Anyway, ukweli unabaki palepale kwamba CAF yenyewe haijitambui, hile si zama za mashindano makibwa kama yale kuamuliwa kwa ponyi za mezani, kam ilovyotaka kufanyika kwa Ethiopia kwenye kinyn'ganyiro cha mwaka huu cha fainali za Kombe la Dunia. Kama CAF, wako makini, ITC isingetoka.Mkuu, sakata la Mazembe lilitokea 2011 huku TMS ilikuwa tayari imeshaanza tangu 1st October 2010. Katika hili, vilabu husika vinavyouziana mchezaji vikikamilisha kuingiza information zao kwenye TMS, ndipo chama cha soka cha nchi anakotoka mchezaji kinatuma ITC kwa chama anachoenda mchezaji. Ishu ya Bokungu ni kwamba Mazembe waliidharau timu yake halisi ya Esperance ambayo ndiyo ilikuwa ina mkataba naye, badala yake wakamnunua kutoka Virunga ambayo nako alikuwa anaichezea kimakosa. Kwa hiyo utagundua kuwa chama cha soka cha DRC kilifanya makosa kumuidhinisha kienyeji bila kujaza TMS na kupewa ITC, lakini bado huo haukutosha kuwa utetezi wa Mazembe kutonyang'anywa point kwani ilikuja kuonekana na CAF kwenye system kwamba alitakiwa afanyiwe uhamisho kutoka Esperance, na sio Virunga. Hivyo hivyo Okwi anatakiwa afanyiwe uhamisho kutoka Etoile, na sio SC Villa. Kwa hiyo TFF inaweza kumuidhinisha kienyeji Okwi acheze Yanga, lakini pale timu yoyote itakapolalamika CAF au FIFA, itakuja kugundulika kwamba vilabu vilivyotakiwa kujaza information kwenye TMS ni Etoile na Yanga, ambapo baada ya information ku-match, chama cha soka cha Tunisia (FTF) kingeituma ITC kwenda chama cha soka cha Tanzania (TFF), jambo ambalo halijafanyika!
Msiwastue Yanga,waacheni ili wacomoro wapate point za bure
Sisi wala hatuhitaji kumtumia Okwi katika mechi nyingine zaidi ya ile ya Nani Mtani Jembe, Jumamosi hii, Simba 'mtalokota' mipira 6 kutoka nyavu zenu.