Okwi (Yanga) vs Besala Bokungu (TP Mazembe)

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,606
20,339
Besala Bokungu alitoka Mazembe, akaenda Esperance ya Tunisia. Mkataba wake na klabu ya Tunisia ulisitishwa na chama cha soka cha nchi nyingine ya Jamhuri ya Congo,ambacho kiliidhinisha uhamisho wake kujiunga na klabu ya Virunga, klabu ambayo baadaye ilimuuza kwa Mazembe.

Okwi alitoka Simba, akaenda Etoile du Sahel ya Tunisia. Pamoja na kuruhusiwa na FIFA kuichezea Villa kwa muda wa miezi 6 tu wakati anatatua matatizo yake na Etoile,
kimantiki mkataba wake na klabu ya Tunisia ulisitishwa na chama cha soka cha nchi nyingine ya Uganda, kwa kuidhinisha uhamisho wake kujiunga na klabu ya Villa na kisha klabu hiyo kumuuza kwa Yanga.

Sasa angalia jinsi Mazembe walivyonyang'anywa point kwa kumchezesha Bokungu:

Reigning African champions TP Mazembe of DR Congo have been disqualified from the Champions League.

The Confederation of African Football (Caf) took action after a complaint from Tanzanian side Simba about the eligibility of Janvier Besala Bokungu.

Mazembe beat Simba 6-3 on aggregate in the second round of the tournament.

Simba will play Morocco's Wydad Casablanca, who lost to Mazembe in the third round, for a place in the group stages of the tournament.

The one-off game will be played at a neutral venue next week.

Mazembe have won the Champions League for the last two years and reached the final of the Club World Cup last season, losing 3-0 to Italians Inter Milan in the final.

Bokungu, a 22-year-old Kinshasa-born defender, was transferred from Mazembe to Tunisian club Esperance in 2007 and rejoined the Congolese club this year.

Reports say he then broke a contract with the Tunis team that runs until June this year, but a Mazembe official insisted the Bokungu transfer was legal.
 
......but a Mazembe official insisted the Bokungu transfer was legal

...Alipoulizwa kuhusu utata wa sakata lake ambalo limefika hadi FIFA, Kleb alisema; "Tumefuatilia kote, hadi kwa wanasheria, na tumefanikiwa kupata hadi ITC yake, nawaambia mashabiki wa Yanga wajue viongozi wao wanafanya kazi, hatuna stori nyingi, sisi tunafanya vitendo, tunafanya kazi kwa siri sana,".
"Na tumepitia sehemu zote, tumeona kabisa tuko sahihi katika kumsajili mchezaji huyu na hakutakuwa na tatizo lolote upande wetu,"alisema.

Yeah, that's nice analogue. Anachosisitiza Bin Kleb ndicho hicho hicho alichokuwa anasisitiza Frederic Kitengie, GM wa Mazembe, lakini ukweli ukajulikana
 
Bado sijaelewa kabisa
Kuelewa hii unahitaji uwe tayari unajua series ya usajili wa Okwi kutoka Simba => Etoile => SC Villa => Yanga, halafu uwe na kumbukumbu ya jinsi TP Mazembe ilivyonyang'anywa ushindi kwa kumtumia mchezaji waliyeuziwa na kuidhinishwa na chama cha soka kingine (FECOFA - DRC) tofauti na kile ambacho mchezaji huyo ana mkataba na klabu iliyo chini yake (FTF - Tunisia)
 
Hii ni kama kufananisha maziwa na tui la nazi. Ingawa rangi vinafanana, ladha na matumizi ni tofauti. Angalia:
1. CAF ni chama kinachopendelea timu za Arabuni, ilivyokuwa makao makuu yake (na kwa hivyo watendaji wake wengi) yako nchi ya Kiarabu, Misri. Waliinyan'ganya TP Mazembe kwa kujua kwamba mshindi wake na Simba angekutana na timu ya Arabuni. Kwa manufaa ya timu hiyo, ni vyema ingekutana na Simba kuliko TP Mazembe. Hujiulizi kwa nini Mazembe wanyan'ganywe pointi wakati usajili wa mchezaji aliyelalamikiwa ulikwishapitishwa na CAF hiyohiyo?
2. Wakati ule hakukuwa na utaratibu wa Matching Transfer System, na kwa hivyo aibu ya pointi za mezani kwa kasoro za usajili ilikuwa bado ikiiandama CAF. Tangu kuanza kwa utaratibu huo, uwezekano wa mchezaji kuhamishwa isivyo halali haipo.
 
...

Mkuu, sakata la Mazembe lilitokea 2011 huku TMS ilikuwa tayari imeshaanza tangu 1st October 2010. Katika hili, vilabu husika vinavyouziana mchezaji vikikamilisha kuingiza information zao kwenye TMS, ndipo chama cha soka cha nchi anakotoka mchezaji kinatuma ITC kwa chama anachoenda mchezaji. Ishu ya Bokungu ni kwamba Mazembe waliidharau timu yake halisi ya Esperance ambayo ndiyo ilikuwa ina mkataba naye, badala yake wakamnunua kutoka Virunga ambayo nako alikuwa anaichezea kimakosa. Kwa hiyo utagundua kuwa chama cha soka cha DRC kilifanya makosa kumuidhinisha kienyeji bila kujaza TMS na kupewa ITC, lakini bado huo haukutosha kuwa utetezi wa Mazembe kutonyang'anywa point kwani ilikuja kuonekana na CAF kwenye system kwamba alitakiwa afanyiwe uhamisho kutoka Esperance, na sio Virunga. Hivyo hivyo Okwi anatakiwa afanyiwe uhamisho kutoka Etoile, na sio SC Villa. Kwa hiyo TFF inaweza kumuidhinisha kienyeji Okwi acheze Yanga, lakini pale timu yoyote itakapolalamika CAF au FIFA, itakuja kugundulika kwamba vilabu vilivyotakiwa kujaza information kwenye TMS ni Etoile na Yanga, ambapo baada ya information ku-match, chama cha soka cha Tunisia (FTF) kingeituma ITC kwenda chama cha soka cha Tanzania (TFF), jambo ambalo halijafanyika!
 
hoja ya msingi hapa ni iwapo TMS ilikwishaanza kutumika, na kama ndio, ilitumika ipasavyo. Sifa mojawapo ya mtandao (network) ni kufananisha takwimu zinazoingizwa na zilioko kwenye database. Kwa hivyo hata kama Villa itaingiza taarifa kuwa Okwi ni mchezaji wake halali, database ya CAF lazima itabaini iwapo ni halali kweli au la. Na huo ndio uzuri wa TMS. Anyway, ukweli unabaki palepale kwamba CAF yenyewe haijitambui, hile si zama za mashindano makibwa kama yale kuamuliwa kwa ponyi za mezani, kam ilovyotaka kufanyika kwa Ethiopia kwenye kinyn'ganyiro cha mwaka huu cha fainali za Kombe la Dunia. Kama CAF, wako makini, ITC isingetoka.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom