Oktoba 29: Kutiki au Kutikisa?

Oktoba 29: Kutiki au Kutikisa?

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
445
Reaction score
553
Siku zinayoyoma kwa kasi kuelekea Oktoba 29, 2025.

Kuna pande mbili kuu zenye mitazamo tofauti kabisa kuhusu nini hasa kinapaswa kutokea siku hiyo. Je, itakuwa siku ya kutiki au kutikisa?

Pande zote mbili zina hoja zao. Upande mmoja unaamini kwamba suluhisho la changamoto za taifa letu lipo kwenye kutiki kura, yaani kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi. Kundi hili lina watu wenye imani na tume huru ya uchaguzi na wale walinzi wa kura (Linda Kura yako). Pia kuna wale ambao wanafuata mkumbo tu, wakiwa wamebebwa na matumaini ya ahadi mbalimbali walizopewa wakati wa kampeni. Imani yao ni kwamba kwa kupiga kura, wananchi watachagua viongozi wanaowataka na hivyo kupata maendeleo wanayoyatamani.

Upande mwingine unaona kwamba uchaguzi pekee hautoshi. Kundi hili linapendekeza kutikisa utawala kupitia maandamano. Ingawa uongozi wa harakati hii bado binafsi siujui, wazo hili linanivutia binafsi. Hoja yao kuu ni kwamba wanasiasa wengi, mara tu wanapoingia madarakani, huwasahau wapiga kura wao na kuanza kufuja mali za umma. Kwao, maandamano ni njia ya kuwaonyesha viongozi kwamba wapiga kura wanajua haki zao na wako tayari kuzitetea. Wananchi wanataka kuona mali za nchi zikisimamiwa kwa umakini na fedha zao zikitumika vizuri, badala ya kutumiwa kuwanufaisha wachache.

Harakati hii ya kutikisa ina mvuto wa pekee kwa sababu:
1.Haina ahadi tupu. Wale wanaounga mkono wako tayari hata kwa maumivu, wakiamini kwamba hakuna maendeleo makubwa bila juhudi za dhati na hata kujitoa mhanga. Wanajua kuwa hii si njia rahisi, lakini wanaamini ni muhimu.

2.Inawakumbusha viongozi wajibu wao- Hili linaweza kusababisha mshtuko na kuwaonesha viongozi kwamba wako chini ya uangalizi wa wananchi. Inawapa changamoto ya kuacha kufuja mali za taifa na badala yake kuelekeza nguvu zao kwenye kuijenga nchi.

3.Inaweza kupunguza matatizo, siyo kuyamaliza- Hali ya nchi ina changamoto nyingi, lakini mojawapo ya kubwa zaidi ni utawala bora na usimamizi wa rasilimali. Hatua yoyote inayolenga kuongeza uwajibikaji inaweza kusaidia, hata kama haitatatua matatizo yote.


Iwe ni kwa njia ya kutiki kura au kutikisa utawala, ujumbe ni mmoja: wananchi wanataka kuona mabadiliko chanya.

Swali muhimu tunalopaswa kujiuliza ni, je, tunataka kuendelea kuwa watazamaji tu au tunataka kuchukua hatua? Huenda njia bora ni kutiki kwa umakini, na wakati huo huo kutikisa kwa kudai uwajibikaji wa viongozi wetu.
 
Hakuna watu wanapitia wakati mgumu kipindi hiki kama ccm, vitambi vinawasumbua na mawazo yamewatinga, tabu tubu aisee!.
 
Back
Top Bottom