OIC yaibuka upya Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OIC yaibuka upya Zanzibar

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngaramu, Apr 1, 2011.

 1. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Suala la Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa (OIC) limefufuka upya, baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutakiwa kutoa msimamo wake kwa kuwa Serikali ya Muungano imeshindwa kujiunga katika jumuiya hiyo.
  Hali hiyo ilijitokeza jana wakati wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walipokuwa wakichangia ripoti ya Kamati ya Fedha, Kilimo na Biashara ya Baraza hilo, iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Salmin Awadh Salmin.
  Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani, Rashid Seif Suleiman, alisema wakati umefika kwa SMZ kutoa msimamo wake kwa sababu Serikali ya Muungano imeshindwa kutekeleza ahadi ya kujiunga na jumuiya hiyo.
  Alisema kitendo cha Serikali ya Muungano kushindwa kujiunga na OIC hadi sasa kimechangia kurudisha nyuma maendeleo ya Zanzibar.
  Mwakilishi huyo aliliambia Baraza kuwa serikali lazima ielezee sera yake kuhusiana na suala hilo kwa sababu yapo mataifa yamenufaika na jumuiya hiyo licha ya kuwa idadi kubwa ya wananchi wake sio waumini wa dini ya Kiislamu.
  Aliyataja mataifa hayo kuwa ni Msumbiji na Uganda ambayo yananufaika na miradi ya elimu na kwamba Zanzibar ingeweza kupiga hatua kubwa ikiwa isingejiondoa katika OIC.
  Zanzibar iliamua kijiunga na OIC wakati wa awamu ya tano ya uongozi chini ya Rais Mstaafu Dk. Salmin Amour Juma. Hata hivyo, baadaye ililazimishwa kujitoa kwenye jumuiya hiyo kwa maelezo kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano na kwa kufanya hivyo bila ruhusa ni kukiuka katiba ya nchi.
  "Miaka 16 serikali ya Muungano imeshindwa kujiunga na OIC, wenzetu Uganda wamenufaika na Chuo Kikuu cha Mbarali," alisema Mwakilishi huyo.
  Suala la OIC limeibuka muda mfupi baada ya Zanzibar kufanya mabadiliko ya 10 ya katiba yake ambapo katika kifungu cha kwanza na cha pili cha katiba hiyo ya mwaka 1984, yanaipa Zanzibar hadhi ya kuwa nchi.
  Kifungu cha kwanza cha katiba ya Zanzibar sasa kinasomeka kuwa Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo vilivyozungukwa na bahari yake, ambayo kabla ya Muungano ilikuwa ikiitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar.
  Kabla ya marekebisho hayo ya katiba, kifungu hicho kilikuwa kikisomeka kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Akizungumzia kero za Muungano, Suleiman alisema kasi ya utatuzi wa kero za Muungano haiendani na ukubwa wa tatizo na kutoa mfano kuwa tangu kuundwa Kamati ya Fedha ya pamoja (JFC) mwaka 2003, hakuna ripoti hata moja iliyotekelezwa.
  Alisema kamati hiyo imefanya kazi ya kupitia vyanzo vya mapato na kutoa mapendekezo yake, lakini ripoti hizo hadi sasa hazijawekwa hadharani na hakuna utekelezaji wowote.
  Naye Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma, alisema serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar inalionea haya kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano. Alieleza kwamba serikali ya awamu ya sita imefanya jitihada kuliondoa suala hilo katika orodha ya mambo ya Muungano na kupitishwa na vyombo vya maamuzi vya Zanzibar, lakini hadi sasa mafuta na gesi asilia hayajaondolewa katika mambo ya Muungano.
  Hamza ambaye alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi wakati ulipopitishwa uamuzi wa kuondolewa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano, alisema suala hilo hatalinyamazia na atakuwa mkali katika kikao kijacho cha Baraza hilo, iwapo litakuwa halijaondolewa.
  "Shughuli itakuja kuwa nzito katika kikao cha bajeti, jitihada zimekwisha kufanywa na serikali ya awamu ya sita, lakini sasa mnalionea haya," alisema.
  Alieleza kwamba ni jambo linaloshangaza kuona gesi asilia ni jambo la Muungano, lakini ni mwaka wa nane sasa tangu ianze kuvunwa Zanzibar imekuwa hainufaiki.
  Alisema mgawo unaotolewa wa asilimia 4.5 kwa ajili ya misaada na mikopo unafaa uangaliwe upya, ili Zanzibar ipate asilimia 11.5 kama ilivyo katika hisa zake za kuanzishwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Akijibu hoja za wajumbe hao, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi, Omar Yussuf Mzee, alisema hawezi kulizungumzia suala la OIC kwa vile halimo katika ripoti ya kamati hiyo.
  Kuhusu Zanzibar kuwa na chombo kimoja cha kukusanya kodi badala ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), alisema mfumo unaotumika hivi sasa una nafuu kwa Zanzibar.
  Alisema mapato yanayokusanywa na TRA yote yanabakia Zanzibar kwa shughuli za maendeleo na kwamba wafanyakazi wa mamlaka hiyo hulipwa mishahara na huduma nyingine na Serikali ya Muungano.
  Waziri Mzee alisema serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali kusimamia kwa ufanisi ukusanyaji mapato hasa yatokanayo na vyanzo vya mapato vya taasisi za serikali.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  tutawapakata kwa kutumia jeshi jwtz labda america iwatete
   
 3. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwinyi Sadallah
  Suala la Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa (OIC) limefufuka upya, baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutakiwa kutoa msimamo wake kwa kuwa Serikali ya Muungano imeshindwa kujiunga katika jumuiya hiyo.
  Hali hiyo ilijitokeza jana wakati wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walipokuwa wakichangia ripoti ya Kamati ya Fedha, Kilimo na Biashara ya Baraza hilo, iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Salmin Awadh Salmin.
  Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani, Rashid Seif Suleiman, alisema wakati umefika kwa SMZ kutoa msimamo wake kwa sababu Serikali ya Muungano imeshindwa kutekeleza ahadi ya kujiunga na jumuiya hiyo.
  Alisema kitendo cha Serikali ya Muungano kushindwa kujiunga na OIC hadi sasa kimechangia kurudisha nyuma maendeleo ya Zanzibar.
  Mwakilishi huyo aliliambia Baraza kuwa serikali lazima ielezee sera yake kuhusiana na suala hilo kwa sababu yapo mataifa yamenufaika na jumuiya hiyo licha ya kuwa idadi kubwa ya wananchi wake sio waumini wa dini ya Kiislamu.
  Aliyataja mataifa hayo kuwa ni Msumbiji na Uganda ambayo yananufaika na miradi ya elimu na kwamba Zanzibar ingeweza kupiga hatua kubwa ikiwa isingejiondoa katika OIC.
  Zanzibar iliamua kijiunga na OIC wakati wa awamu ya tano ya uongozi chini ya Rais Mstaafu Dk. Salmin Amour Juma. Hata hivyo, baadaye ililazimishwa kujitoa kwenye jumuiya hiyo kwa maelezo kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano na kwa kufanya hivyo bila ruhusa ni kukiuka katiba ya nchi.
  “Miaka 16 serikali ya Muungano imeshindwa kujiunga na OIC, wenzetu Uganda wamenufaika na Chuo Kikuu cha Mbarali,” alisema Mwakilishi huyo.
  Suala la OIC limeibuka muda mfupi baada ya Zanzibar kufanya mabadiliko ya 10 ya katiba yake ambapo katika kifungu cha kwanza na cha pili cha katiba hiyo ya mwaka 1984, yanaipa Zanzibar hadhi ya kuwa nchi.
  Kifungu cha kwanza cha katiba ya Zanzibar sasa kinasomeka kuwa Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo vilivyozungukwa na bahari yake, ambayo kabla ya Muungano ilikuwa ikiitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar.
  Kabla ya marekebisho hayo ya katiba, kifungu hicho kilikuwa kikisomeka kuwa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Akizungumzia kero za Muungano, Suleiman alisema kasi ya utatuzi wa kero za Muungano haiendani na ukubwa wa tatizo na kutoa mfano kuwa tangu kuundwa Kamati ya Fedha ya pamoja (JFC) mwaka 2003, hakuna ripoti hata moja iliyotekelezwa.
  Alisema kamati hiyo imefanya kazi ya kupitia vyanzo vya mapato na kutoa mapendekezo yake, lakini ripoti hizo hadi sasa hazijawekwa hadharani na hakuna utekelezaji wowote.
  Naye Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura, Hamza Hassan Juma, alisema serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar inalionea haya kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano. Alieleza kwamba serikali ya awamu ya sita imefanya jitihada kuliondoa suala hilo katika orodha ya mambo ya Muungano na kupitishwa na vyombo vya maamuzi vya Zanzibar, lakini hadi sasa mafuta na gesi asilia hayajaondolewa katika mambo ya Muungano.
  Hamza ambaye alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi wakati ulipopitishwa uamuzi wa kuondolewa suala la mafuta na gesi asilia katika orodha ya mambo ya Muungano, alisema suala hilo hatalinyamazia na atakuwa mkali katika kikao kijacho cha Baraza hilo, iwapo litakuwa halijaondolewa.
  “Shughuli itakuja kuwa nzito katika kikao cha bajeti, jitihada zimekwisha kufanywa na serikali ya awamu ya sita, lakini sasa mnalionea haya,” alisema.
  Alieleza kwamba ni jambo linaloshangaza kuona gesi asilia ni jambo la Muungano, lakini ni mwaka wa nane sasa tangu ianze kuvunwa Zanzibar imekuwa hainufaiki.
  Alisema mgawo unaotolewa wa asilimia 4.5 kwa ajili ya misaada na mikopo unafaa uangaliwe upya, ili Zanzibar ipate asilimia 11.5 kama ilivyo katika hisa zake za kuanzishwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Akijibu hoja za wajumbe hao, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi, Omar Yussuf Mzee, alisema hawezi kulizungumzia suala la OIC kwa vile halimo katika ripoti ya kamati hiyo.
  Kuhusu Zanzibar kuwa na chombo kimoja cha kukusanya kodi badala ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), alisema mfumo unaotumika hivi sasa una nafuu kwa Zanzibar.
  Alisema mapato yanayokusanywa na TRA yote yanabakia Zanzibar kwa shughuli za maendeleo na kwamba wafanyakazi wa mamlaka hiyo hulipwa mishahara na huduma nyingine na Serikali ya Muungano.
  Waziri Mzee alisema serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali kusimamia kwa ufanisi ukusanyaji mapato hasa yatokanayo na vyanzo vya mapato vya taasisi za serikali.
   
  Attached Files:

Loading...