Habari za kawaida
Posted Date::2/2/2008
Shule zenye majina ya viongozi hoi mtihani kidato cha nne
Na Joyce Mmasi
SHULE za sekondari zenye majina ya viongozi, zimeonekana kufanya vibaya ukilinganisha na heshima za majina ya viongozi hao.
Matokeo ya Shule ya Sekondari ya Nyerere Memorial yenye wanafunzi 131 waliofanya mtihani; ni wanane tu waliofaulu, wakati 123 wakifanya vibaya.
Katika shule hiyo mwanafunzi mmoja alipata daraja la kwanza, la pili watano na tatu wawili, 83 daraja la nne na 40 waliambulia patupu.
Katika Shule ya Sekondari Amani Abeid Karume, wanafunzi waliofeli ni 68 wakati waliofaulu ni tisa tu. Shule hii mwaka 2004 ilikuwa miongoni mwa shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa.
Shule ya Ali Hassan Mwinyi waliofeli ni wanafunzi 97 waliofaulu ni 11 tu wakati katika shule ya Dk Omary Ali Juma waliofeli ni watoto 14 na waliofaulu ni 13.
Katika Shule ya Sekondari Nelson Mandela imefaulisha wanafunzi wanane na 61 kufanya vibaya, huku shule ya Zakia Meghji iliyokuwa na watahiniwa 84, ni 13 tu waliofaulu huku 71 wakianguka vibaya.
Shule ya Moringe Sokoine ilijumuisha watahiniwa 104, waliofeli ni 61 huku 43 wakifaulu. Shule ya sekondari ya Kawawa waliofanya vizuri ni 10 na waliofeli ni 89.
Sekondari nyingine ni yenye jina la JK Nyerere ambapo kati ya wanafunzi 204 waliofanya mtihani 75 walifeli na 129 kufanya vizuri. Shule ya Dk Ali Mohamed Shein iliyokuwa na wanafunzi 21 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, ni wanafunzi wawili tu waliofaulu.
Shule nyingine ni Mererani Benjamin Mkapa ambayo imefaulisha mwanafunzi mmoja tu na kuacha wengine 26 wakifeli wakati Shule ya Frederick Sumaye imefaulisha wanafunzi 45 na 52 kufeli mitihani hiyo.
Vile vile katika shule yenye jina la J.J Mungai wanafunzi 143 wamefeli na waliofaulu ni 27.
Orodha hiyo ya shule zenye majina ya viongozi inafungwa na Benjamin Mkapa High School ya Dar es Salaam ambayo imefelisha wanafunzi 173 na 193 kushinda kati ya daraja la kwanza hadi la tatu.
Baadhi ya viongozi walio hai na wengine marehemu, wamekuwa na tabia ya kuzibatiza au kuruhusu baadhi ya shule kupewa majina yao, lakini viongozi hao hawafuatilii maendeleo ya shule hizo.
Ni wazi kuwa, kufanya vibaya kwa shule hizo kwa miaka na miaka, si tu kunashusha heshima za viongozi hao, bali pia kunatoa fursa ya wao kujitazama na kuanza kuziangalia shule hizo mara kwa mara. Matokeo ya mitihani Uk 26.