Ofisi ya TRA Kigoma 'yamchefua' Waziri Jafo

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
2.jpg
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameonyeshwa kufadhaishwa kwa kukosekana kwa afisa wa TRA katika Kituo cha Kibiashara cha Pamoja ambacho lengo lake ni kurahisisha shughuli za kibiashara kwa wananchi wa Wilaya ya Kigoma kwa kupata huduma zote za uwezeshaji wa biashara.

Kutokana na hali hiyo waziri Jafo ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Kigoma kufanya ufuatiliaji wa haraka ndani ya siku nne ili kituo hicho kiweze kuwa na Wadau wote wa kutoa huduma na wananchi waweze kupata huduma ya kuanzisha na kuratibu biashara zao kwa haraka.

Inaelezwa kuwa kwamba TRA walishafika kituoni hapo na kuahidi kuleta Afisa mmoja lakini hadi leo bado jambo hilo halijafanyika hivyo kuleta usumbufu kwa wafanya biashara wanaohitaji huduma kutoka katika kituo hicho.
 
Heading ingekuwa Waziri Jafo "ashangazwa" maana hii awamu unaweza ukashangaa TRA nao wanamshangaa Waziri jafo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom