Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 962
- 1,978
The Tanganyika Law Society
The Bar Association Of Tanzania Mainland
22 SEPTEMBA 2025.
TAARIFA KWA WANACHAMA WA TLS NA WATEJA WANAOFIKA KUPATA HUDUMA MAKAO MAKUU YA TLS.
Leo, Ofisi ya Makao Makuu ya TLS imezingirwa na askari. Tunaiona hali hii kama "ulinzi" ulioongezwa, japokuwa tungependa nguvu na rasilimali hizi zingeelekezwa kuwatafuta na kuwaokoa ndugu zetu waliopotezwa ambapo kwa siku moja tu wote wangeweza kurejeshwa na kuungana na familia zao.
TLS itaendelea kutimiza wajibu wake kwa ueledi na bila woga, upendeleo, hofu wala husda katika kuhakikisha Utawala wa Sheria na Haki za Binadamu zinasimamiwa na kuheshimiwa.
Kwa sasa, tunaendelea na taratibu za mazungumzo zilizokwisha anza na mamlaka stahiki ili kuhakikisha vitendo na vituko vinavyofanywa na baadhi ya askari wa Polisi ndani ya maeneo ya Mahakama au wakati wa utimizwaji wa majukumu mbalimbali ya kisheria dhidi ya Mawakili na Wananchi vinakomeshwa mara moja.
Tunawasihi mawakili wote kubaki na tahadhari na kutochokozeka kwa uchokozi huu wa makusudi unaofanywa dhidi yao na Jeshi la Polisi na kutii maelekezo ya Baraza la Uongozi tuliyowasilisha kwenu kwa maandishi kuhusu umuhimu wa kutoa nafasi kwa mazungumzo yaliyokwisha anza.Ni jukumu letu sisi viongozi kushughulikia jambo hili kwa haraka na kwa wakati na kutoa mrejesho kwenu kwa wakati. Umoja wetu na nidhamu yetu ni silaha kubwa ya kulinda heshima ya taaluma yetu na haki za wananchi.
HATUTAOGOPA KUSIMAMIA HAKI NA KUPINGA DHULUMA.
Imetolewa na Baraza la Uongozi la TLS
BONIFACE A. K. MWABUKUSI
RAIS-TLS