Ofisi ya Republican yarushiwa bomu Marekani

Ofisi ya Republican yarushiwa bomu Marekani

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Ofisi moja ya chama cha Republican katika jimbo la North Carolina imeharibiwa na moto huku jengo lililo karibu yake likipakwa rangi ya nembo inayopinga chama cha Republican,mamlaka imesema.

QA.jpg


Chupa iliojazwa mafuta yanayoweza kushika moto ilirushwa katika dirisha la makao makuu ya chama cha Republican kaunti ya Orange,chama hicho kimesema.

Mkurugenzi wa chama cha Republican, Dallas Woodhouse alisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa,na kwamba tahadhari ya kiusalama imetumwa katika afisi nyengine za chama hicho.

''Wanachama wa Nazi walio katika chama cha Republican ni sharti waondoke mjini''.

QB.jpg


Mgombea wa Democrat Hillary Clinton ameandika katika mtandao wake wa Twitter kwamba shambulio hilo ni ''la kutisha na halitakubalika''.

Lakini Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump alionekana akiwalaumu wafuasi wa chama cha Democrat kwa kutekeleza kitendo hicho.

''Wanyama wanaomwakilisha Hillary Clinton huko North Carolina walirusha bomu katika ofisi yetu ya kaunti ya Ornge kwa sababu tunashinda'',alisema katika mtandao wake wa Twitter.

Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom