Kwenu wanajamvi naomba kufahamishwa kama ni sahihi baada ya Bunge kuvunjwa rasmi Mawaziri wanaweza kuendelea na Uwaziri. Ninavyofahamu kwa kuwa Uwaziri wa sasa ni mpaka uwe Mbunge na tayari Bunge limevunjwa hivyo hakuna Mbunge tena, vivyo hivyo hakuna Mawaziri tena.
Lakini tunachoshuhudia ni Mawaziri kutekeleza Uwaziri kinyume na Katiba ambayo naamini inamtaja Katibu mkuu wa Wizara katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi. Kama wanaendelea na kama wamepata ridhaa ya Rais basi Rais amevunja Katiba na nadhani wanataaluma wa sheria nchini wataliangalia hili kwani kwa kiasi fulani kutekeleza kwao uwaziri kunawapa fursa ya kukipigia kampeni chama chao.