ofisi ya CAG ifungwe

Madcheda

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
422
69
Taarifa kwa Umma, Jumanne 10 Mei 2011
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ifungwe!

[/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Kwa miaka kadhaa sasa, serikali imeshindwa kufuatilia matokeo na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali, na hivyo kukosa uwezo wa kuboresha usimamizi wa fedha za umma. Kwa mwaka 2010 kwa mfano, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali ametoahati yenye mashaka kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Hati hiyo ina maana kwamba kuna mambo kadhaa yanayogharimu kiasi cha shilingi 21 bilioni yalikuwa hayajafanyiwa kazi na wizara kwa kuzingatia kanuni za uhasibu zinazokubalika.
Wakati kiasi hiki kikishangaza kwa ukubwa wake, ikilinganishwa na uwezo mdogo ulioonyeshwa na wizara kiutendaji, kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita Mkaguzi Mkuu alihoji matumizi ya shilingi 215 bilioni (sawa na shilingi 22 bilioni kwa mwaka). Matatizo makuu manne ya kiuhasibu yanayozalisha mzigo wa maswali kwa wizara ni pamoja na; gharama zinazohusiana na matibabu ya nje ya nchi shilingi 6.3 bilioni, kulipwa mishahara kwa wafanyakazi hewa shilingi 1 bilioni, kutorejeshwa kwa masurufu ya muda mrefu shilingi 6.5 bilioni na matumizi ya fedha yenye hati pungufu shilingi 107 bilioni.
Hata hivyo si sahihi kuilaumu Wizara ya Afya pekee kwa kuwa maswali hayo pia yanaigusa serikali kwa ujumla. Katika ripoti ya mwaka 2009/10, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu amehoji kiasi cha shilingi 786.5 bilioni pamoja na kutoa hati yenye mashaka kwa Wizara, Idara na Mashirika mbalimbali, Sekretarieti za Mikoa na Utawala pamoja na Balozi zipatazo 22 kati 108. Malipo ya zaidi ya shilingi 382 bilioni yalimelipwa bila ya kuwa na nyaraka husika, shilingi 2 bilioni malipo ya mishahara kwa wafanyakazi hewa, pia kiasi cha shilingi 161 bilioni zikiwa ni za madeni ya muda mrefu. Kwa upande wa serikali za mitaa mwenendo ni huu huu.
Mambo yote haya yanaendelea kuibua maswali juu ya juhudi za serikali za kuboresha usimamizi na kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma. Wajibu wa uangalizi wa Mkaguzi Mkuu unaendelea kupungua kutoka katika uhalisia wake kutokana na kuzalishwa kwa ripoti ambazo zimebeba mambo yale yale kila mwaka huku Bunge na serikali zikishindwa kufanya lolote. Mkaguzi mwenyewe anasema "
[/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Katika ripoti ya ukaguzi wa mashirika ya umma ya mwaka ulioishia tarehe Juni 2008 jumla ya mapendekezo 15 yalikuwa yametolewa.Hadi kufikia tarehe ya kuandika ripoti hii mapendekezo yote 15 yalikuwa hayajatekelezwa ipasavyo[/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]".
Ripoti za Bunge za mapitio ya ukaguzi pia zimeshindwa kuleta nidhamu, uadilifu na uwajibikaji katika matumizi na usimamiaji wa fedha za umma. Kamati tatu za ukaguzi za Bunge (za Hesabu za Serikali, Hesabu za Serikali za Mitaa na Hesabu za Mashirika ya Umma) zimekuwa zikijadili ripoti ya ukaguzi wa hesabu ingawa mazungumzo hayo hayajazaa matunda yoyote. Sababu ya msingi inaweza kuwa Kamati za ukaguzi za Bunge zinakosa nguvu ya kusimamia na kukosoa kazi zisizotekelezwa na mamlaka husika kama zilivyoainishwa na Mkaguzi Mkuu. Hali hii inaibua maswali juu ya uhalali wa matumizi ya fedha za umma kuendeshea ofisi ya taifa ya ukaguzi.
Kulingana na vitabu vya Bajeti vya mwaka wa fedha 2010/11, kiasi cha shilingi bilioni 30 zilitengwa kwa ajili ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Kwa kuwa matokeo ya zoezi zima la ukaguzi hayachukuliwi kwa uzito wake na Bunge pamoja na wizara husika, hivyo Sikika inapendekeza kwamba, Fedha hizi za umma zingeweza kutumika katika kuboresha maisha ya Watanzania. Kwa mujibu wa bei za Bohari Kuu ya Dawa ya mwaka 2010/11 chandarua kimoja kinagharimu kiasi cha shilingi 3300 na vifaa vya kupimia VVU vinauzwa shilingi 180,000. Kwa hiyo, shilingi bilioni 30 kwa ajili ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi zinaweza kununua vyandarua milioni tisa vyenye saizi ya (1050x220x56 sentimita) au vifaa vya kupimia VVU vipatavyo 167,000.
Hivyo basi Sikika, inatoa wito wa kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuboresha uadilifu, nidhamu, na uwajibikaji katika fedha za umma au kufungwa kabisa kwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
[/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]
Mr. Irenei Kiria
Mukurugenzi wa Sikika, P.O.Box 12183 Dar es Salaam,
Simu: +255 222 666355/57, Nukushi: 2668015, Barua pepe: info@sikika.or.tz, Tuvoti: www.sikika.or.t

source; SIKIKA
[/FONT]
[/FONT]
 
Back
Top Bottom