Leo ndo nimefanya hitimisho la kuthibitisha uozo wa maofisa wa masoko na biashara hapa halmashauri ya manispaa ya Kibaha mjini, naomba mkuu wa mkoa na mkurugenzi afuatilie suala hili.
Ipo hivi;
Mwaka jana nilienda kufuatilia leseni ya biashara pale manispaa nikapewa form na kuandikiwa documents za kuandaa, nikawaeleza kuwa nataka kufungua duka la rejareja kwa vitu vya majumbani yaani(vitu vya Umeme, vyombo vya kupikia, maplastiki sabuni, vocha et) nikaambiwa na ofisa aliekuwepo niandae laki mbili kwa kila kitu.
Nikaondoka kutafuta nyaraka alizo niorozeshea,baada ya wiki mbili nikaenda sikumkuta badala yake nikamkuta ofisa mwingine mwanamke akakagua document zangu na kunitaka kwanza nimpatie elfu 20,000 ili anifanyie faster, sikujua ni faster ya namna gani nikampa hela hyo na kumuuliza risiti, akaja juu na kwa hasira akiniambia kama nataka risiti nikalipe benki, nikamkubalia kwenda kulipa benki kwa sababu sio mbali na pale, Njuweni branch.
Alivyoona nipo hivyo akaniambia kuwa anatoka anaenda likizo, nisirudi mpaka uchaguzi uishe. Nilisikitika sana lkn sikuwa na jinsi nikaondoka.
Tarehe 4/01/2016 nikaenda nikamkuta msichana mwingine, baada ya maelezo yangu akaniambia nimpatie hizo documents, bila kulikuwa kumepungua passport size ikanibidi nikapige then nirudi, akaniambia niandae 20,000 ya kulipia.
Niliporudi muda wa kazi ulikuwa umeisha, nikaenda tarehe 10/01/2016 pia nikaambiwa na binti mwingine mpya niandae 150,000 nikalipe. Nikamuuliza, mbona kila ofisa anataja bei yake? Kwani hamna catalogy inayoonyesha bei? Akaniambia bei inapangwa kulingana na maelezo, nikamuuliza maelezo si tayari yapo kwenye form na sahihi zote zipo?
Baada ya mahojiano hayo akaniambia hata hivyo maofisa hawapo wote wameenda kwenye mkutano na waziri wa ardhi Maili moja, ndg Lukuvi, nikaondoka.
Sasa leo tarehe 13/01/016 nimeenda nikakutana na maofisa wengine wanaume na bei mpya kabisa ya leseni. Baada ya mabishano nikaona wamekasirika na kuniambia nirudi ofisi ya serikali ya mitaa akagonge muhuri tena maana imekaa mda mrefu sana.
Nikawaambia mda mrefu umesababishwa na nyinyi, nakuja mnaleta sababu zisizo na mbele wala nyuma, nikija hiyo siku ingine mnaleta sababu zingine, ila kuna mtu nje akaniambia wanataka rushwa, ukiwapa 20,000 tu mda huohuo unapata na kuondoka. Nikamwambia kuwa kwangu hata tank hawapati na leseni nitapata.
Sasa naomba waziri, mkuu wa mkoa, mkurugenzi fuatilia hili haya kama utataka nikuthibitishie namba yangu ni 0718186686. Nakuonyesha mtu mmoja mmoja na kauli zao nimezirecord, tunarudishana nyuma!