Ofisa kilimo achapwa bakora na wakulima

Ofisa kilimo achapwa bakora na wakulima

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Zaidi ya wakulima 19 waliovamia vyanzo vya maji katika bwawa la Mwanzugi wilayani Igunga wamemchapa bakora Ofisa Kilimo wa Kata ya Igunga, Jamila Issa kwa kuwapiga picha.

Tukio hilo lilitokea jana Jumapili ofisa huyo alipokwenda kuangalia utekelezaji wa agizo alilotoa Agosti 27 la kuwapa siku 14 wakulima hao wawe wameondoka katika bwawa hilo.

Ofisa huyo amesema alienda eneo hilo akiwa amefuatana na baadhi ya viongozi wa mtaa kukagua iwapo wakulima wameondoka lakini waliwakuta wakiendelea na kilimo kwenye vyanzo vya maji.

“Nilipofika eneo hilo nilikuta wakulima zaidi ya 19 wakiendelea na kilimo, baadhi wakipanda nyanya na mahindi. Nilianza kuwapiga picha kupata ushahidi, walipobaini walinishambulia kwa fimbo huku viongozi niliofuatana nao wakitimua mbio,” amesema ofisa kilimo Issa.

Amesema baada ya kuanguka, wakulima walitimua mbio na majembe yao na fahamu zilipomrudia alienda kituo cha polisi kuchukua fomu kwa ajili ya matibabu ambayo aliyapata katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga na aliruhusiwa kurejea nyumbani.

Hata hivyo, amesema hataogopa kufanya kazi na kuwachukulia hatua wote watakaoendelea kulima kwenye vyanzo vya maji.

Mtendaji wa Kata ya Igunga, Robert Mwagala amesema Polisi kwa kushirikiana na raia wema watawasaka wakulima waliomshambulia ofisa kilimo huyo.

Diwani wa Igunga, Charles Bomani amesema kitendo kilichofanywa na wakulima hao hakikubaliki, hivyo ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Baadhi ya wakulima waliotii agizo la kuondoka kwenye bwawa hilo wamelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka juu ya watu waliofanya ukatili huo.

Mkazi wa Kata ya Igunga, Idd Jackson amesema ni aibu na fedheha kumshambulia kiongozi akitekeleza majukumu yake, hivyo ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe kwa waliohusika.


Chanzo: Mwananchi
 
Hahaha dah umenifanya niwakumbuke wale watafiti waliochomwa moto na wanaichi kwa kujia ni nyonya damu

Ila wanaichi bana tena ambao hawajasoma au ambao hawana elimu ukiwaambia fanyeni hivi hawakuelewi ila sasa wakipatwa na matatizo ndo wa kwanza kulalamika hawajawahi kumuona ofisa

pole sana ofisa siku nyingine nenda na diwani, mgambo na kil mtu wasije wakakuchoma moto ukafa
 
Mazoezi nayo ni muhimu,angekuwa yuko fit si angekimbia ili kuepusha madhara zaidi...
 
Jambo kama hili haliwezi kuvumilika na ni la kulaani kwa nguvu zote,,, leo wamemchapa afisa kilimo wakichekewa kesho diwani, mwenyekiti na hatimae mkuu wa Wilaya...
Wakulima waliofanya kitendo hicho ni wavunjaji wa sheria na wanapaswa kutiwa nguvuni mara moja..
Pole sana Afisa kilimo uliyekutwa na tukio hilo..
 
Huyu anatafta kiki tu.

[emoji124]‍♂️naenda zimbobo.
 
Jambo kama hili haliwezi kuvumilika na ni la kulaani kwa nguvu zote,,, leo wamemchapa afisa kilimo wakichekewa kesho diwani, mwenyekiti na hatimae mkuu wa Wilaya...
Wakulima waliofanya kitendo hicho ni wavunjaji wa sheria na wanapaswa kutiwa nguvuni mara moja..
Pole sana Afisa kilimo uliyekutwa na tukio hilo..
kweli kbs hao wawafunge tu
 
Back
Top Bottom