Ofisa Habari wa CHADEMA aandaa press ya Kuivuruga ACT

Ofisa Habari wa CHADEMA aandaa press ya Kuivuruga ACT

kailakarama

Member
Joined
Aug 30, 2014
Posts
73
Reaction score
30
Chama cha demokrasia na maendeleo(chadema),kimetuhumiwakusuka mkakati wa kukuvutia chama cha ACT-Tanzania kwa kutumia baadhi ya wanachama wa chama hicho.

Taarifa ambazo zimelifikia gazeti hili Dar-es-salaam jana,mmoja wa viongozi wa chama hicho,alisema kuwa wanahisi chadema wanacheza mchezo mchafu wa kuhakikisha ACT-Tanzania inaingia kwenye mgogoro.

Chanzo hicho (jina tunalo),kilisema kwa hali ilivyo kuna kila dalili ya Chadema kuhusika ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano uliofanywa juzi na baadhi ya wanachama wa ACT-Tanzania ambao wanajitambulisha kwenye vyombo vya habari kama waasisi wa chama hicho.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa taarifa waliyonayo ni kwamba mmoja wa maofisa wa habari wa chadema,ndiyo alihusika kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kwa vinatakiwa kwenda kwenye mkutano huo wakiamini baada ya habari kutoka watakuwa wamefanikiwa kutimiza malengo yao.

Hata hivyo,chanzo hicho hakikuwa tayari kutaji jina la ofisa anayetuhumiwa kuhusika katika mkakati wa kuichafua ACT-Tanzania.
Alipotafutwa kwa njia ya simu, ofisa habari wa chadema, Tumaini Makene ili kuzungumzia tuhuma hizo, alisema hawezi kuzizungumzia maana yupo mkoani ambapo alitaka kufahamu ni nani alitoa madai hayo.
Chanzo: Gazeti la Jambo Leo tarehe 13/11/2014.
 
Sources Jambo Leo. Juma Pinto?

Haya...
 
kama wana uhakika kwanini wasimtaje kwa jina huyo afisa habari wa cdm? huku ni kutapatapa
 
Source Muuza Sembe!!! CHADEMA haina haja ya kuihujumu chama ambacho hakina hata uwezo wa kuongoza timu ya mpira... achene akina Nyakarungu et al wadai mgao wa ESCROW walizo ahidiwa...
 
Wametumika vibaya na kutelekezwa na baba yao CCM, sasa wanataptapa.ACT dhambi ya usaliti inawatafuna.
 
Wanatapatapa hao wavurugane wenyewe wasingizie Chadema? Wakumbuke Chadema nimpango wa Mungu... Dhambi ya usaliti inawatafuna hao wachumia tumbo
 
Poor ACT,nipo Igoma Mwanza ,Chagulani akitoboa hila zake nitajiua.
 
Kumbe gazeti lenyewe JAMBO LEO? Lile linalomilikiwa na wafadhili wa hilo genge la wachumia tumbo!
 
Wasaliti wanasalitiana wanasingizia cdm hiyo ndo dhambi ya usaliti
 
Tumaini makene ni mhuni sana ACT ni chama kidogo sana leo anahangaika kukihujumu kazi kweli.
 
Tumaini makene ni mhuni sana ACT ni chama kidogo sana leo anahangaika kukihujumu kazi kweli.

Usifananishe watu wa Chadema na hao hapo Lumumba, Soma chanzo cha habari kama ndio mbinu zenu basi zimebumm jaribuni tena
 
ukimwangalia usoni tu utagundua haraka kuwa mwigamba ana njaa kali.
 
Back
Top Bottom