Official: Wimbo mpya ya Roma Mkatoliki - Zimbabwe

Rudia tena kusikiliza, kuna sehemu kasema hakuona nyota kwenye shoulder japo anajua ni solider... Ulikuja mwenyewe au ulipewa order

Mungu wa Paulo ama John mnayemuita Yohana hahahahaha katisha sana Roma.. Kuna sehemu pia kasema alipokuwa hakujua kama ni saa nne ama Saanane.... Wapi Ben wa Saanane
 
Huyu Roma ni GENIUS

Kwa misatari hii minne kama hujaelewa bac wewe ni kilaza, maana amejibu kila kitu.

1. Mungu wa Paulo ndio Mungu wa Daudi na ndio Mungu wa John wanayemwita Yohana wa Yahudi.

2. Na ripoti ya upelelezi
Je ni vipi akiiteka mtekaji?

3. Walioniteka hawakuja na Noah
Ni uvumi na visanga
Ila kutekanatekana huu ni uhuni wa kishamba.


4.Mi sikuona nyota kwa shoulder
Ila najua wewe ni soldier
Ulikuja mwenyewe ama ulipewa order.
 
Mungu wa Paulo ndio Mungu wa Daudi na ndio Mungu wa John wanayemwita Yohana.a .......john tunamwita yohana,,,,,yohana alikua mbatizaji na alibatiza watu kwa maji......ha ha haaaa huyu roma huyu kwahiyo haya majipu ni kwamba .......makinikia tuyatungie mistari
 

Waloniteka hawakuja na Noah/
Ni uvumi na visanga/
Ila kutekana tekana huu ni uhuni wa kishamba/


Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja/
Maana sote lengo letu kuijenga Tanzania moja/

Mi sikuona nyota kwa shoulder/
Ila najua wee ni soja/
Ulikuja mwenyewe au ulipewa order/


Soma mwendelezo wa hizo lyrics mzee utaelewa. Kakataa Noah ila gari hajalitaja ila unaweza kutabiri kitu akilini ukiendelea na hizo lyrics za chini
 
Ndungu weka mfumo mwepesi tudownload hiyo ngoma kali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyimbo nzuri hakika! PlayStation zote za TV na Radio zitatekwa na hii nyimbo,bado mtaani kwa bodaboda na waingiza nyimbo kwenye flash.Ni hit song kwa kweli
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…