Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,082
- 828,874
Ni wangapi waliiangalia sinema ya Sometimes in April? Tuombe sana Mungu na sisi tusije tukaja kutengeneza sinema ya October to remember ..! Na kama ikitokea hivyo basi iwe kwa heri na si kwa kumbukumbu za kutisha na kutia simanzi.
Leo ni tarehe moja mwezi wa kumi.. Mwezi uliongia kwenye historia za mataifa ya Tanganyika na Zanzibar kwa kuondokewa na mmoja wa waasisi wa Taifa la Tanzania. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mchonga meno hapo mnamo tar 14.10.
October hii inaweza kuwa tofauti kabisa na October nyingine zote na siku ya tar 14 ya kumbukizi ya kifo cha Mwalimu Nyerere inaweza kutumiwa na wananchi kufanya jambo kubwa sana.
Maono mbalimbali, tabiri, mijadala mbalimbali na hali halisi vinaonesha kwamba kuna mwamko mkubwa sana wa kutaka mabadiliko chanya ya kisiasa kati ya wananchi wa mataifa yote mawili ya Tanganyika na Zanzibar.
Mwamko huu pamoja na mengine yote ni hitaji la nyakati..! Mojawapo ya vitu ambavyo huwa havizuiliki basi ni mahitaji ya nyakati.. Wakati ukitimia lililopangwa kuwa HUWA!
Mahitaji ya nyakati ni sawa na maji yanayosafiri hasa baada ya mvua kubwa kunya! Kamwe usijaribu kuyazuia haya maji kwakuwa
Mosi hutaweza.. I mean hutafanikiwa!
Pili kama utaweza kuyazuia basi ni kwa muda tuu.
Tatu yatakuletea madhara makubwa sana utakapojaribu kuyazuia yasipite yatakapo ama yaingie mahali na yakose pa kutokea
Ndani ya mwaka kuna miezi 12 lakini kiroho kila mwezi una tafsiri yake! Kwa miezi inayoishia na na ember hiyo ni miezi ya mabadiliko ama pando la mabadiliko!
September iliyoishia jana tuliiona wote ilivyokuwa imepanda na kuchochea mbegu ya mabadiliko.. Hiyo mbegu itamea October na November unaweza kuja kuwa mwezi mpya utakaobeba mengi mapya yawe mazuri ama mabaya.
All in all hatuombei tuje kutengeneza sinema ya Sometimes in November!
Bado tuna muda wa kutafakari, kutengeneza na kubadili maamuzi kwa amani kwa maelewano na kwa ushirikiano! Bado tuna nafasi ya kujifunza historia na kwa waliotutangulia.. Hatuhitaji kuwa na haraka kwakuwa hata hizo haraka tulizozitumia huko nyuma hapo awali hazikutufikisha popote!
Tukiamua kuwa na tafakuri kuu Tukaacha kiburi
Tukaacha ego
Tukaacha craving
Tukaacha kujiona sisi ni bora kuliko wao
Tukaacha yote mabaya yanayouseta uumbaji wa Mwenyezi Mungu, Oktober hii itapita salama nasi tutaondoka kwa heshima na historia itatuweka mahali pazuri pa kukumbukwa vema!