October 14 iwe sikuku ya ubaguzi Duniani

October 14 iwe sikuku ya ubaguzi Duniani

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2012
Posts
2,977
Reaction score
1,900
Ndugu zangu ubaguzi unatafuna Dunia.
1.Mwislamu na Mkristo kama wapo nchi moja kama hawapo, kama ni waislam basi Shia na Suni,
2.Mzungu na Weusi, kama hawapo ni Mzumgu na myahudi, tukiendelea hivi ni mpaka mwisho ndugu na ndugu kubaguana.

Hotuba kama hii haipo Dunia ni mwalimu pekee aliitoa hapa Tanzania. dhambii hii inalitafuna kila taifa KWA sasa hakuna mwenye hauweni.

Nimekaa na kutafakari kuwa siku ya baba wa Taifa iwe sikukuu ya ubaguzi Duniani. Baba wa taifa alikuwa muumini Mkuu wa Upendo wa dhati. Kumuenzi ni kukumbuka yale aliyotenda tu !


JK Nyerere
""‎"Watu wazima wamezungumza Muungano, kwamba tuuvunje au tuendelee. Ilikuwa ipo hatari ya kuvunjika na wala haijaisha. Watu wamezungumza Uzanzibari, na baadhi ni viongozi wetu, wanajivunia Uzanzibari. Nadhani wengine wanafikiria hata kujitenga. Wapo si wengi; lakini wapo. Kujitenga maana yake ni kuvunja nchi ivunjike tusiwe na nchi moja, tuwe na nchi mbili. Ni jambo linalozungumzwa. Tunataka kiongozi na viongozi watakaoelewa hivyo. Huku kuzungumza Uzanzibari si fahari. Si jambo la fahari. Hatima yake tutavunja nchi. Zanzibar, mtu mwenye akili hawezi kufikiri Uzanzibari ni fahari: hana akili.


Hawezi akautukuza Uzanzibari kwa kujiita 'sisi Wazanzibari' na 'wao Watanganyika'.


Nadhani ile ina usalama ndani yake. Kwamba Uzanzibari ule, Utanganyika ule una usalama ndani yake. Hatima yake Zanzibar itajitenga. Zanzibar ikijitenga kutokana na ulevi tu; sisi Wazanzibari na wao Watanganyika wakumbuke kwamba Muungano ndio unaowafanya wanasema 'sisi Wazanzibari' 'wao Watanganyika'. Nje ya Muungano, hawawezi kusema hivyo: kuna 'wao Wapemba' na 'sisi Waunguja'.


Nataka mjue hivyo. Nje ya Muungano hakuna 'sisi Wazanzibari' 'wao Watanganyika'. Hakuna. Kinachowafanya mjiite 'sisi' ni ubaguzi wa kuwabagua Watanganyika. Wakiisha kuwabagua Watanzania Watanganyika, ile dhambi ya ubaguzi, haifi inaendelea. Dhambi ya ubaguzi ukisha kuitenda inaendelea: ni kama ukila nyama ya mtu utaendelea kuila. Mtamaliza mtatengana na Watanganyika halafu, mara mtakuta kumbe 'sisi' 'si Wazanzibari'. Kuna 'Wapemba' na 'Waunguja'. Wapemba watapata msukosuko kidogo aaolololo!


Mtakuta kumbe kuna Wazanzibari na Wazanzibara! Hamtakaa salama. Hamwezi mkakaa salama baada ya kutenda dhambi ya kuwabagua watu wa nchi yenu ile ile moja mkawaita 'wale wao' na 'hao sii'. Dhambi ile haiishii hapo. Ndivyo historia ilivyo; ni sheria ya historia siyo sheria ya Mwalimu Nyerere. Huwezi kufanya ubaguzi wa namna hiyo halafu dhambi ile ikuache hapo hapo. Hapana itakuandama."
 
Back
Top Bottom