OCT 2020 Namuona mwenyekiti wa NEC akimtangaza Rais kupita bila kupingwa

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,610
13,160
Wakuu ni dhahiri sasa tutarajie kutokuwa na kampeni kwa nafasi ya Uraisi na makamu. Wagombea vyama pinzani wataunga juhudi wengi kwa kufika bei na endapo mbishi atatolewa kwa kutokidhi vigezo.

Ushuhuda wa hili ni matamko, matendo, hukumu ya Membe kamati kuu CCM na uchaguzi uliopita serikali za mitaa.Watanzania tuamke kila mmoja kwa nafasi yake tuseme hapana, hili ni taifa letu sote haya mambo ya Kifalme sio sehemu ya utamaduni wetu.
 
Hivi
Screenshot_20200228-124057.jpeg
 
Majaliwa ya nchi hii kwa siku za usoni yatakuwa zaidi mikononi mwa mataifa makubwa, wao ndio watakaoamua hatima ya nchi hii.

Kama wataridhia dhuluma zinazofanywa na hii serikali kwa watu wake basi watawala watakuwa wamepona lkn kama watakataa kuridhia basi zama za ccm kuitawala nchi hii zitakuwa zinaelekea ukingoni.

Utegemezi wa serikali nyingi duniani kwa hayo mataifa makubwa unazilazimisha mataifa mengi duniani kucheza mziki wao wapende wasipende na Tanzania sio exception.
 
Ndio maana yake na kipindi cha awamu ya pili bunge zima litakuwa la CCM , ushindi wa Uraisi Tanzania haupatilani kwa karatasi upinzaji mkilielewa hili halitawasumbua
 
Inawezekana hujui Katiba au Sheria ya uchaguzi. Hakuna Rais anayeweza kupita bila kupingwa.
Acha unafiki! Fanya masihara tu utaenda kuchomwa moto! Halafu utajua ulichokuwa unachofanya Duniani ni kipi. Nazungumzia haki sizungumzii siasa.
 
Inawezekana hujui Katiba au Sheria ya uchaguzi. Hakuna Rais anayeweza kupita bila kupingwa.
Ni kweli katiba inasema kama kuna mgombea mmoja wa urais watu watapiga kura za ndio au hapana. Lakini ukishakuwa na mgombea mmoja ni sawa na mgombea huyo kupita bila kupingwa. Hii ni kwa sababu wapinzani hawataruhusiwa kuweka mawakala ktk vituo vya kupigia kura, kura watahesabu na kujumlisha watakavyo na watatangaza matokeo wanayopenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukombozi utaanzia Zanzibar, kutakua na kiza kinene kabla hakujapambazuka. Ni lazima kile cha zamani kife ili kutoa nafasi kwa kipya kuzaliwa.
Inshallah
 
Akipitishwa bila kupingwa atapinduliwa ndani ya mwaka mmoja. Tanzania haina ubavu wa kuhimili vikwazo vya kiuchumi.
 
Wakuu ni dhahiri sasa tutarajie kutokuwa na kampeni kwa nafasi ya Uraisi na makamu. Wagombea vyama pinzani wataunga juhudi wengi kwa kufika bei na endapo mbishi atatolewa kwa kutokidhi vigezo. Ushuhuda wa hili ni matamko, matendo, hukumu ya Membe kamati kuu CCM na uchaguzi uliopita serikali za mitaa.Watanzania tuamke kila mmoja kwa nafasi yake tuseme hapana, hili ni taifa letu sote haya mambo ya Kifalme sio sehemu ya utamaduni wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Checheee.
 
Hata ikitokea hivyo ccm kukabidhi nchi kwaupinzani inatakuwa ngumu sasa yaani kuliko wakabidhi ni bora waingie msituni

Back
Top Bottom