JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
MKUU wa Polisi Kiteto, SP Fadhili Luoga, ametoa masaa 48 kwa wafugaji wa jamii ya kimasai waliofanya uhalifu kujisalimisha.
Uhalifu uliofanywa ni kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima, pamoja na kuwajeruhi wakulima hao.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Namelock Wilayani humo, Luoga àlisema, kitendo cha wafugaji kuwapiga wakulima bila sababu halikubaliki.
"Huwezi kuingiza mifugo kwenye shamba la mkulima kisha unamwachia maumivu..unampiga kwanini umpige? amefanya kosa gani?"alihoji Luoga
" Sasa imefikia hatua mmeanza kupigana wenyewe kwa wenyewe ni aibu... kwani juzi watu waliopigana mikuki walipigana kwa sababu gani haya ni mambo ya aibu"
Àlisema hivi sasa hakuna sababu ya kupigana kwasababu ya kugombea mabua...busara zitumike unapohitaji mabua ya mwenzako tena usubiri awe ameondoa mazao yake sio ulimkuta unapiga tu.
Katibu Tarafa ya Kibaya, Zulfa Laiza alieleza wananchi hao kuwa ameagizwa na MKUU wa Wilaya kuwa, jamii hiyo iache kutembeza mifugo barabarani kwani ina haribu barabarani.
" Nimekuja kuwapa ujumbe kutokana kwa MKUU wa Wilaya ya Kiteto kuwa, Wafugaji muache kutembeza mifugo yenu barabarani sambamba na kuchunga kwenye hifadhi ya Emboley Murtangos"
Hili ni agizo na tayari tumesha tengeneza boma kwaajili ya kuhifadhi mifugo itakayokamatwa mpaka itakapolipiwa àlisema Laiza
Tumetengezea barabara kwa gharama kubwa sana km 88 ya thamani ya 4.6 bil kwa ufadhili wa Wamarekani kwanini tuiharibu? alihoji Laiza
Kwa upande wake Michael Lepunyat Diwani wa kata ya Namelock aliridhia kukamatwa mifugo hiyo àlisema wameshatoa Elimu isipokuwa wafugaji wanakaidi.
Mwisho