Styvo254
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 246
- 226
Hamjambo Wote WanaJamii,
Kama wengi wenu mjuavyo, magari na mitambo ya kisasa ina husisha mfumo wa diagnosis katika sehemu mbali mbali. Wamiliki wa magari na madereva bila shaka sio wageni na taa ya Check Engine au MIL (Malfunction Indicator Lamp). Lakini, swali muhimu ni wangapi wanaelewa mfumo wa OBD una maana gani kwenye chombo?
Engine na mifumo mbali mbali ya kisasa ina husisha umeme wa digital au elektroniki katika uangalizi(monitor), udhibiti(control) na utekelezi(actuate) wa utenda kazi wake. Hii ni kwa usalama, ubora na wepesi wa gari au mtambo. Mtandao huu wa umeme pia umewezesha mawasiliano kati ya ECU au 'bongo' za mifumo tofauti kwenye chombo kw mfn breki (ABS) na engine na transmission. Mawasiliano haya yanawezesha usawazishaji wa tukio mara moja bila dereva kuhusika kama vile gari linapoteleza kwa barbara telezi, breki uhusika kupunguza na kusawazisha mwendo wa kila gurudumu ili kudhibiti mwendo NA mwelekeo wa chombo, wakati huo huo gear pia inashushwa ili kuyapa magurudumu uzito kwenye barabara.
Sijasahau mada wapendwa, ila ni kuieleza poa zaidi.
Mfumo wa On Board Diagnosis ni aina ya mtandao, rekodi na mawasiliano maalum ya kiufundi kwa zile bongo za mifumo ya chombo. Hii yahusisha kusoma matatizo(faults) yaliopo kwenye mfumo, kuangalia(monitor) utendakazi wa mfumo na pia kulazimisha utendakazi kwa ajili ya ukaguzi(test) na utekelezi(actuation); hii ya mwisho ni kwa vifaa kwenye mfumo ambazo uhusika na usalama, udhibiti maalum au utendaji kazi unaohitaji taarifa(data) maalum kwenye mfumo na kwa hivyo ni lazima iwekwe au inukuuiwe na mfumo wa kiufundi.
Kutoka na hayo maelezo hadi sasa waweza kuona kua mfumo wa OBD una nukuu matatizo yanapotokea, lakini sio rahisi hivyo! Lazima bongo lihesabu ni mara ngapi tatizo linatokea kw kila chombo kitumiwavyo (Key Cycle). Na pia kama tatizo linahusika na utumizi au mazingira ya mda huo. Ni kwamba sio kila tatizo litawasha MIL, kusema kutowaka kwa MIL sio kutokua na tatizo.
Watengenezaji vyombo hivi walikusudia tukio la Service litahusisha Diagnosis ya chombo ili kukagua hali ya mfumo kwa wakati mzuri - kabla ya kuharibika! Na pia gari linapotoa taarifa tata likaguliwe kwa kina katika mazingira take ya kazi na matumizi; hii ni wazi kwa engine za electronic injection diesel kama vile D4D(Toyota) na DI(Mitsubishi).
Kinacho nishinda hadi sasa ni mafundi wenzangu wameshachukia teknolojia hii ya kurahisisha kazi na kuiogopa wakidai ni kuwapotezea ajira, Upumbafu Mtupu! Ukichelewa usidai umetengwa - ni lazima fundi ajiongeze kitaaluma kwa kua ulimwengu unajoingeza kila kuchao.
Shukran sana na Karibuni sana!