Obama Kulipwa Dola Laki 4 (USD400,00) Kwa Speech Ya Afya Mwezi September

alvinroley

Member
Sep 30, 2016
71
251
Rais wa Zamani wa USA Barack Obama amekubali ombi la Taasisi ya Cantor Fitzgerald LP ya kumpa Dola Laki 4 (USD400,000) ili atoe speech kwenye HealthCare Conference mwezi September mwaka huu itakayofanyika Wall Street.
Jamaa ana takriban siku zisizopungua 100 nje ya ofisi ya White House na anategemea kupiga mkwanja huo kwa speech ya dakika 30.
1493287884937.jpg
 
kama Billion moja hivi ya madafu kwa rate ya sasa just kuongea tu
daaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Rais wa Zamani wa USA Barack Obama amekubali ombi la Taasisi ya Cantor Fitzgerald LP ya kumpa Dola Laki 4 (USD400,000) ili atoe speech kwenye HealthCare Conference mwezi September mwaka huu itakayofanyika Wall Street.
Jamaa ana takriban siku zisizopungua 100 nje ya ofisi ya White House na anategemea kupiga mkwanja huo kwa speech ya dakika 30.
View attachment 501754
Obama angeamua kwenda kufanya kazi Wall St. badala ya kugalagala kwenye ma ghetto ya Chicago angepiga hela ndefu zaidi ya hiyo miaka mingi sana iliyopita.

Millions of dollars. Akiwa mdogo sana.

Kwa hiyo mwachieni tu apige hela sasa kwa sababu kashamaliza kufanya kazi ya serikali ambayo ina mshahara mbuzi.

Imagine sasa anapiga dola laki nne kwa speech moja. Alivyokuwa rais huo ni mshahara wake wa mwaka mzima.
 
Bila shaka hizo dolari anaingiza kiasi kwenye taasisi yake ya Obama Foundation
 
ndio wabongo tunapo shindwaga hapo, wenzetu USA mtu hatajiriki akiwa Rais bali akisha staafu, Bill Clinton alimaliza urais akiwa na madeni ya USD milion 12, ila sisi mtu akiingia kwenye urais ndio ana faidika, Obama baada ya kustaafu ndio ata enjoy pesa at his own expense na taifa kama taifa halipati hasara na kujitajirisha kwa viongozi
 
Bila shaka anastahili na hasa ukizingatia Sera yake ya Obama care iliwanufaisha wamarekani wengi wasio na vipato.
 
Mkuu huko wall street ndo huwa wanabeba hela hadi kwenye sandarusi..?? Maana kwa Maelezo yako huko hela nje nje kama mtu alivyokuwa anachota pale mkomboz benk.
Obama angeamua kwenda kufanya kazi Wall St. badala ya kugalagala kwenye ma ghetto ya Chicago angepiga hela ndefu zaidi ya hiyo miaka mingi sana iliyopita.

Millions of dollars. Akiwa mdogo sana.

Kwa hiyo mwachieni tu apige hela sasa kwa sababu kashamaliza kufanya kazi ya serikali ambayo ina mshahara mbuzi.

Imagine sasa anapiga dola laki nne kwa speech moja. Alivyokuwa rais huo ni mshahara wake wa mwaka mzima.
 
Mkuu huko wall street ndo huwa wanabeba hela hadi kwenye sandarusi..?? Maana kwa Maelezo yako huko hela nje nje kama mtu alivyokuwa anachota pale mkomboz benk.
Sandarusi haitoshi.

Leo nilikuwa nasoma Wall St. Journal mtu anapewa dola za Kimarekani milioni 189. Tena huyo kaharibu kazi anaondoka.

Sasa utabeba sandarusi ngapi hapo?
 
Ina maana licha ya mdororo wa kiuchumi uliopo duniani kwa kipindi hiki bado watu huko wall street wana ona hela y Obama kama vijisenti tu na hela ya mboga kwa hiyo Jamaa aliyeharibu kazi na kulipwa 189$ M.
Sandarusi haitoshi.

Leo nilikuwa nasoma Wall St. Journal mtu anapewa dola za Kimarekani milioni 189. Tena huyo kaharibu kazi anaondoka.

Sasa utabeba sandarusi ngapi hapo?
 
huyu dereva wetu wa Roli sijui atakuwa analipwa shilingi ngapi huyu? au huyu hata akipewa mbuzi sawa tu anaenda kutiririka vibaya vibayaaa
Huyu labda apewe na clouds kwenye kipindi cha gea abibu arushe mipasho...kwa mipasho tu,aaah huyu mbona yupo vizuri!!!
 
Back
Top Bottom