Obama atakuwa Rais wa kwanza kutengeneza programu ya kompyuta

Msamiati

R I P
Mar 6, 2011
1,072
0
obama1.jpg

Katika uzinduzi wa wiki ya masomo ya sayansi ya kompyuta, Jana rais Barack Obama alishiriki bega kwa bega katika kuhamasisha vijana wadogo dunia nzima kujifunza jinsi ya kutengeneza programu za komputa (Computer Programming).


Akizungumza kabla ya tukio hilo rais Barack Obama alisema, "Sayansi ya kompyuta sio kitu cha kustaajabisha kama inavyodhaniwa, hutakiwi kuwa mtumiaji tuwa vitu, tengeneza vitu.

Tumia angalau saa moja kujifunza teknolojia inayogusa kila nyanja ya maisha yetu. Hivyo ndivyo unavyoweza kuandaa uwezo binafsi utakaohitajika kwa ajili ya maisha yako ya baadae.


Katika uzinduzi huo Rais Obama alialika zaidi ya vijana 30 wenye umri wa kati kutoka katika miji ya Newark na Brooklyn, New York na kushirikiana nao katika tukio maalum la utengenezaji wa programu linalofahamika kama"Hour of code".

Katika hatua hiyo Raisi Obama, ameungana na kauli iliyowahi kutolewa na Marehemu Steven Jobs mwaka 2012 enzi za uhai wake katika mahojiano na vyombo vya habari aliposema, "Everybody in this country should learn how to program a computer, because it teaches you how to think."

Kitendo hiki cha rais Obama kuonesha uzalendo katika teknolojia pia kimetoa hamasa kubwa miongoni mwa vijana wengi wanaojifunza masomo ya sayansi ya kompyuta pamoja na kuamsha viongozi wengi wa kiafrika ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa nyuma kwenye kuhamasisha mataifa yaokupiga hatua katika teknolojia.

By Msamiati


 

Msamiati

R I P
Mar 6, 2011
1,072
0
Viongozi wetu inabidi waige mfano huu wa kushiriki kwa vitendo katika kuhamasisha maendeleo
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
15,824
2,000
Yaani...ashidwe na 'hello world'...!? mnamuonea wa makwetu.
========================================
Mbali na kasoro nyingine za kiutawala, na kupongeza kwa hili Hussein.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom