Obama apingwa kwa maandamano makubwa usa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Obama apingwa kwa maandamano makubwa usa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Sep 14, 2009.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,451
  Likes Received: 22,404
  Trophy Points: 280
  Maelfu Waandamana Marekani Kupinga Serikali ya Obama
  [​IMG]
  Maelfu waliojitokeza jana kupinga utawala wa Obama
  Maelfu ya watu wakibeba mabango yanayopinga utawala wa rais Obama na mageuzi yake katika mfumo wa afya anayotaka kuyafanya, waliandamana jana hadi katika maeneo ya ikulu ya Marekani.

  "Utoaji mimba sio mageuzi katika Afya" lilisema bango moja huku bango jingine lililobebwa na mhamiaji nchini Marekani toka Ukraine lilisema "Nilishauchoka ujamaa kwenye muungano wa soviet USSR".

  Mtoto Quinn Ryan, 11, alisimama katikati ya mtaa wa Pennsylvania Avenue, karibu na sehemu ambayo Obama na mkewe Michelle walitembea siku ile yenye baridi wakati Obama alipoapishwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Marekani.

  Ryan alikuwa amebeba bango linalosema "Nimezaliwa bure, nitalipishwa kodi mpaka nitakapofariki".

  "Hali mbaya ya uchumi imeathiri nyumba nyingi, imetubidi tuandamane ili hali isiwe mbaya zaidi" alisema dada yake Ryan mwenye umri wa miaka 13 ambaye naye alikuwa amebeba bango lake tofauti.

  Maandamano hayo yalilenga kupinga utawala wa rais Obama na kukishtumu chama cha democratic kwa kutaka kuigeuza Marekani nchi ya kijamaa.

  Maandamano hayo yaliandaliwa Freedomworks, taasisi inayopigania kushushwa kwa viwango vya kodi na uchumi huria ikipinga mabadiliko ambayo rais Obama anataka kuyafanya katika masuala ya bima katika mfumo wa afya wa Marekani.

  Waandaaji wa maanandamano hayo walisema awali katikati ya wiki kuwa walitegemea kati ya watu 20,000 na 30,000 toka kila kona ya Marekani kuhudhuria maandamano hayo.

  Maelfu waliitikia wito wa maandamano hayo wakiwa na mabango mbali mbali kuonyesha upinzani kwa rais Obama.

  Waandamanaji wengine walibeba mabango yaliyosema "You lie" wakikumbushia maneno aliyosema seneta wa Arizona toka chama cha Republican, Joe Wilson ambaye alimwambia Obama muongo wakati alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye bunge la kongresi la Marekani kuhusiana na mageuzi anayotaka kuyafanya kwenye mfumo wa afya wa Marekani.

  Maandamano hayo yaliisha mapema kabla ya muda uliopangwa kutokana na idadi ya watu kuwa kubwa sana kuliko uwezo wa eneo hilo.

  Inakadiriwa watu milioni mbili toka kona mbali mbali za Marekani walihudhuria maandamano hayo.


  SOURCE:- NIFAHAMISHE.COM
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  pamoja na kipinga sera za Obama laikini pia kuna mkono mkubwa wa ubaguzi ndani yake,
  tatizo lingine la binadamu ni wepesi mno kusahau, yeye Obama sio aliyeyumbisha uchumi bali ni Bush lakini watu wameshasau na kuanza kumwita jamaa ni muhongo,
  kuwa mweusi ni taabu ktk hii dunia?
   
Loading...