Oa/olewa na unaempenda bila kuangalia mali wala elimu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,775
Habari za leo wapendwa,

Katika pita pita yangu nilikutana na wanandoa waliodumu kwa karibu miaka 35. Mume akiwa na miaka 64 sasa hivi. Walioana mume akiwa na miaka 29 na mke alikuwa na umri wa miaka 25 hawa walikuwa wapenzi walioishi mtaa mmoja, na walifanikiwa kupata watoto wawili. Sasa hivi ni babu na bibi.

Kisa cha kuandika ka ujumbe haka ni kuwa bwana yule akiwa na umri wa miaka 35 alipata ajali mbaya sana ya gari hali ilikuwa tete na baada ya tiba za muda mrefu amebaki amepooza kutoka kifuani kwenda chini.

Anaweza kula, kujisafisha uso lakini hawezi hata kujisogeza mwenyewe wala kusukuma haja kubwa kutoka. Kila baada ya siku mbili mke inabidi amwingize mkono na kuota uchafu ulio kwenye utumbo mkubwa. Yule mama aliniambia anampenda mume wake kama alivyompenda miaka 40 iliyopita enzi anamchumbia, tena ananiambia alikuwa kijana aliyesumbua wengi kwa uzuri wake.

Pamoja na pesa nyingine za miradi yao mke alikuwa mwajiriwa na ndiyo kwanza amestaafu na kulipwa mafao. Nimejiuliza tu kama huyu mama asingeenda kwa mapenzi angeyamudu yote haya?
 
Sky umeongea vizur hapo ila wako wangap waweza kufanya hivi Leo. may Allah bless me with one kwakwel maana kwa hal hi I n 10 out of 100
 
Back
Top Bottom