Oa mwanamke mwenye elimu

Mambo yamebadilika malezi Yamekuwa magumu Sana Kwa watoto wa kizazi hiki ni kweli ni muhimu kuangalia mtu wa kuzaa nae sio tu mwanamke hata mwanaume ulikosea step ndo umeangamia mazima maana uzao ukishakuwa wako haibadilishiki
Kabisa!!!

Ila acha tuendelee na machaguzi yetu ya tall & handsome, wallet nono, wowo etc. tutashtuka giza likishaingia.
 
Mtu wakuzaa nae watoto lazima achaguliwe kwa umakini, bila hivyo unaweza juta sana mbeleni.

Ila kufika Form 4 sio kigezo maana hata kilaza anaweza akafika.
Ni kweli lakini at least anakuwa ana kitu flani kichwani tofauti na ambaye hajafika kabisa

Mkuu mimi najihusisha na masuala ya watoto..naona kabisa ni namna gani baadhi ya wanaume wameta hasara kubwa katika suala zima malezi ya msingi ya watoto wao

Na asilimia kubwa ya hao wanaume wameoa darasa la saba A na B

Be careful mkuu..choose wisely
 
Nilitamani nikuonyeshe mama fulani amezaa na wanaume watatu wote professionals !!! kuna injinia, daktari na mwanasheria na akafanikiwa kuzaa watoto na kila mmoja wa hao wanaume watoto wote walisoma na wa mwisho kisomi ni daktari.
Mama hadi leo ukimwambia andika ' a' mnagombana!! japo kusoma anaweza kidogo.
Wakati fulani lilia amani tu kwenye ndoa mengine yana settle kirahisi sana mkiwa na amani.
 
Hao hao wanaume wanaoambiwa waoe wanawake wenye elimu, hizo elimu zenyewe hata haziwasaidii ujinga mtupu, unakuta mtu na master yake lakini anayoyafanya unajiuliza huyu mwanaume shule alienda kufanya nini hiki mikichwa au mkia haeleweki, wasio na elimu ndiyo wanamwendesha, vigezo si elimu tu pia akili ya kuzaliwa na malezi, wanaume wenyewe na elimu zao wala haviendana ni hovyo hovyo tu.

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
[emoji817] sure
 
Ikiwa hujasoma
 
Na je wale waliofaulu darasa la 7 vizuri ila familia ikakosa pesa za kumwendeleza tunawaweka kundi gani?je tuwaweke kwa wale wasio na ufahamu mkubwa kwa sababu ya kushindwa kuendelezwa?hivi mtoa uzi umefikiria vzr kweli au umerukia tu kuanzisha uzi au umejiona wewe CV yako imeshiba sanaa...la! hashaa huu si uungwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…